Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea

Cement sio bidhaa ya kufungia godown
 
Waziri wa Viwanda hajateuliwa! Sijui huyo atakayeteliwa atakauja na sera gani! Maaana sera ya Tanzania ya viwanda imeishia wapi.
 
Umeitendea haki mada.
Waziri wa Viwanda na yule wa Ujenzi waanze na hili tatizo.
 
Umeitendea haki mada.
Waziri wa Viwanda na yule wa Ujenzi waanze na hili tatizo.
Yaah wa ujenzi itabidi arejee kufanya tathmini ya mahitaji yote ya cement kwenye miradi yote ya ujenzi ya serikali halafu wa viwanda aangalie uwezo wa viwanda kuzalisha hayo mahitaji. Hii miaka miwili ijayo wasipofanya kazi zao vizuri, tunaingia kwenye crisis au kuna hatari ya hii miradi kusimama
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu, baba yangu mkubwa alinunuaga mifuko ya cement ya kutosha akafungia ndani, sasa ile sehemu sijui ilikuwa na unyevu unyevu, zile cement karibu zote zilikuwa majabali. ... Umetoa point nzuri sana mkuu
Afu Mwandishi anakuja kutafuta habari juu ya kupanda kwa bei.
Nikammwuliza bei elekezi IPO? Ni sh. Ngapi? Hajui

Nikamwambia akaiulize serikali ilishindwaje kumruhusu Dangote auze 5000 hadi 8000 kwa 50kg kama kweli inamjali mwananchi.

Pia akaulize viwanda kama vinaendelea kuzalisha inaenda wapi. Mwezi wapili huu unaenda kukata baadhi ya waliolipia cement hawajapata
 
Sukari Na Mafuta Ya Kupikia Bei Ilipanda Serikali Ikawa Inapiga Propaganda Mwijage Anazurura
Naona Cement Nayo Inaivua Nguo Serikali
Wanasema Ipo Lakini Haionekani Wakuu Wanahaha
Wafanyabiashara Wamekaza Tu 🤨😑😏😐
 
Hii issue ni crisis kubwa kuliko inavoonekana. Inaonekana kama simple hivi.. ila ni issie nzito
 
Mkuu ishu ni upungufu katika uzalishaji na sio usambazaji. Hata serikali ikiingi haitasaidia tatizo
 

Serekali ya CCM ipunguze kodi? Upo Sirius mkuu?

Hawa watu hawajawahi kabisa kumjali mwananchi wala mfanyabiashara. Zaidi ya kujijali wao tu.
 
Short term measure, waruhusu cement ya nje kuuzwa nchini.

Angalizo
Miradi yote mikubwa ya ujenzi wawe na mikataba (inayofahamika bayana na serikali) na viwanda vyetu vya ndani

Gap, lifidiwe na import kuhudumia "household sectror"
Hii itasaidia "win win" kwa viwanda vyetu vya ndani na walaji binafsi.

Hilo la kuyumba kwa shilingi, watumie sera za kifedha na mikataba ya ushirikiano na wenzetu wenye surplus cement ikiwezekana within EA

Hatua za muda mrefu, waongeze uwezo wa ndani wa uzalishaji kwa kupanua/kufungua viwanda
 
Kabisa mkuu...


Pia ili kudhibiti speculation kwa bidhaa nyeti kama hizo. Serikali inaweza kuweka kanuni kama kuzuia Ajenti mmoja kuwa na mzigo unaozidi mfano asilimia 20 ya usambazaji/mahitaji ya mkoa fulani.

Hii itasaidia hao wenye tamaa kushindwa kumiliki soko
 
Niko pamoja na wewe mkuu!

Kumbe ukiacha U Lisu huwa unakuwa na akili

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Jokes tu mkuu
 
Umeshauri vizur mkuu, uchawi upo kwenye utekelezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…