Serikali, hata haya hamyaoni?

Serikali, hata haya hamyaoni?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hivi serikali kwa kimya chetu mnadhani mmetushawishi? Hivi hata haya siyo ujanja ujanja wenu usio kubalika?

1. Malipo ya shule vyuo vikuu tunakolipa kupitia loan board 100% + interest. Kwa maana vyuo vya umma havina tofauti na vyuo binafsi.

2. Malipo ya hospitali ambapo dawa, kumwona daktari, kulazwa na hadi mortuary ni kulipia kibiashara kama ilivyo kwenye hospitali binafsi.

3. Sasa mnataka kushurutisha bima ya afya mkidai kuwa mmeona wazima na wagonjwa lazima wawe na bima eti kwa sababu mnapata hasara.

VIDEO: Serikali yafumua masharti saba bima ya afya kwa wote

Haya yote bila hata kugusia tozo za simu za Mwigulu na makando kando lukuki yenye kuhusiana na rushwa dhidi yetu huko TRA, Polisi, Mahakamani, LATRA, Ardihi, mahospitali, nk.

Hivi uwekezaji wetu nchini kama wananchi, walipa kodi na wadau kwenye taasisi na mali za umma uko wapi?

Kwamba maisha yaendelee hivi siku zote? Aaaah wapi!

Kwani ni onyo lipi ambalo hamkupewa?

Tofauti na kutesa kwa zamu nyie siku moja mtawajibika kama walamba asali na kuchonga mizinga.

-----

Serikali haipo kwa maslahi yetu bali kufanikisha upigaji wao
 
Serikali imezidiwa na mzigo wa madeni, inakopa kila siku, hakuna namna mwananchi ataacha kuumia kwa uzembe wa serikali husika, hizo huduma zinazolipiwa ni matokeo ya uzembe wa serikali yenyewe, wanachojua wao ni kuchukua 10% kwenye mikataba.
 
toa ushahidi
 
Hakikisha uyasemayo ni facts, na pia points zako ni dhaifu sana.

Wakati wa Elimu bure kwa wote na mambo mrngine yanaanza kuwa magumu kwa ulimwengu na uchumi wake. Bima inakuwa lazima dunia nzima na sio TZ tu.

Tufanye kazi kuwajengea watoto wetu tusingojee vya bure.
 
Ni muda muafaka sasa kwa waganga wa tiba asili za mitishamba kujitokeza gharama za hospitalini zimekuwa kubwa Sana na vipato vya wananchi ni vidogo sana
 
Watu tunalipa kodi na wengine wamelipa kodi maisha yao yote. Zingatia viwango na wingi wa kodi na tozo mbalimbali.

Mali za umma (hospitali, shule nk za umma) haziwezi kuwa sawa na binafsi. Gharama za taasisi za umma haziwezi kuwa sawa na za taasisi binafsi.

Wawekezaji kwenye mali za umma ni sisi ambao pia ni wadau.

"Tunataka au tumezoea vya bure?" Kauli hii tumeisikia mara ya kwanza hivi majuzi. Nyie ndiye washauri wake? Kwani wajibu wa serikali kwa wananchi ni nini?

Kauli hizi ni ukakasi mtupu na hazina mwisho mwema. Hapa chini ni mwendelezo wa kauli hizo:

Kwamba: “Wataalamu wakaona wanaoumwa na wasioumwa wote wajiunge ...'

VIDEO: Serikali yafumua masharti saba bima ya afya kwa wote
 
Hivi serikali kwa kimya chetu mnadhani mmetushawishi? Hivi hata haya siyo ujanja ujanja wenu usio kubalika?

1. Malipo ya shule vyuo vikuu tunakolipa kupitia loan board 100% + interest. Kwa maana vyuo vya umma havina tofauti na vyuo binafsi.

2. Malipo ya hospitali ambapo dawa, kumwona daktari, kulazwa na hadi mortuary ni kulipia kibiashara kama ilivyo kwenye hospitali binafsi.

3. Sasa mnataka kushurutisha bima ya afya mkidai kuwa mmeona wazima na wagonjwa lazima wawe na bima eti kwa sababu mnapata hasara.

VIDEO: Serikali yafumua masharti saba bima ya afya kwa wote

Haya yote bila hata kugusia tozo za simu za Mwigulu na makando kando lukuki yenye kuhusiana na rushwa dhidi yetu huko TRA, Polisi, Mahakamani, LATRA, Ardihi, mahospitali, nk.

Hivi uwekezaji wetu nchini kama wananchi, walipa kodi na wadau kwenye taasisi na mali za umma uko wapi?

Kwamba maisha yaendelee hivi siku zote? Aaaah wapi!

Kwani ni onyo lipi ambalo hamkupewa?

Tofauti na kutesa kwa zamu nyie siku moja mtawajibika kama walamba asali na kuchonga mizinga.

-----

Serikali haipo kwa maslahi yetu bali kufanikisha upigaji wao
Sera inasema hivyo Ni mpaka ibadilike ndo ufanyike vinginevyo..

Kila kitu tukitaka bure ,Kodi za kugharamia hayo zipo?

Cheap is expensive
 
Mkuu sera inasema:

Kwenye taasisi za umma tulipie kama ilivyo kwenye taasisi binafsi?

Zingatia elimu ya juu, hospitali nk malipo ni total cost + interest.

Hapa chini si kauli yangu:

“Wataalamu wakaona wanaoumwa na wasioumwa wote wajiunge ndiyo maana kwenye muswada mkaona ukitaka leseni ya udereva uwe na bima ya afya, pasi ya kusafiria, leseni ya biashara, kitambulisho cha uraia, namba ya mlipa kodi hivi vyote tukavifungamanisha kwa kujifunza kwa nchi zilizofanikiwa."

Inatakiwa pesa kutoka kwetu hata kutokea tulikowekeza wenyewe Ili iende wapi? Kwa walamba asali?
 
Ni muda muafaka sasa kwa waganga wa tiba asili za mitishamba kujitokeza gharama za hospitalini zimekuwa kubwa Sana na vipato vya wananchi ni vidogo sana
Niliona kule temeke wananchi wanalalamika gharama kubwa za matibabu, sijui kumwona daktari, vipimo, dawa na hiyo ni hospitali ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wananchi, kwenye vyuo vikuu vya umma vijana wanalipa sawa na vyuo binafsi kupitia loan board, yaani haionekani tofauti kwamba hiki ni chuo cha umma na hiki ni binafsi......wakianza kazi loan board wanawalundikia deni hadi milioni 30 kwenye salary slips zao.........yaani huduma ambazo zinatakiwa zitolewe na serikali kupitia kodi sasa na zenyewe zimekuwa za kumnyonga mwananchi........hii serikali ya kukopakopa imekuwa mzigo kwa wananchi.​
 
Usisahau pia kuwa bungeni bajeti za taasisi za umma vikiwemo vyuo vya umma inatolewa kwenye fuko kuu litokanalo na kodi.

Taasisi za binafsi wamewekeza wenyewe from scratch na hakuna bajeti.

Walamba asali na jamaa zao wakiwamo kina Mkirindi wako pale, pakimulikwa wanang'aka ati kuwa hoja ni dhaifu.

Bila shaka hoja madhubuti ni wao kuendelea kulamba asali bila mkwaruzo.
 
Ushahidi umetapakaa nchi nzima ajabu unaniambia nitoe ushahidi!

Au wewe ni kipofu unatumia nukta nundu kuingia jf?!

Yale yale ya wenye kutaka wapigiwe 113 kwanza kama vile wao macho hawana.
 
Serikali imezidiwa na mzigo wa madeni, inakopa kila siku, hakuna namna mwananchi ataacha kuumia kwa uzembe wa serikali husika, hizo huduma zinazolipiwa ni matokeo ya uzembe wa serikali yenyewe, wanachojua wao ni kuchukua 10% kwenye mikataba.
Na wanvyozidi kukopa, ndivyo kiasi cha marejesho ya hiyo mikopo kinazifi kuongezeka.

wakiendelea hivi, wataanza kukopa ili kulipia mikopo. Sitashangaa kama wameshafika hapa.
 
NInakazia:

"wakiendelea hivi, wataanza kukopa ili kulipia mikopo."

Kazi ya kupokwa nchi na kuwa wakimbizi wa ndani tunayo.
 
Back
Top Bottom