Serikali hii ya Magufuli itakuwa na ubavu wa kugomea masharti magumu ya Wachina ilhali wanataka kukamilisha miradi hii ndani ya miaka mitano?

Mambo haya ya kufanya vitu bila mipango iliyopo kwenye bajeti imeigharimu sana nchi.
 
Tusihukumu mapema ebu tuipe serikali yetu pendwa miaka 2 harafu tuone!
 
Wachina si wabaya wakati wanatuhumiwa na Internal Labour Organisation ILO kwa kukiuka sheria za kazi na haki za binadamu katika makampuni yao ya Afrika karibu yote.
Hii inatokana na Viongozi wetu mafisadi kununuliwa
 
Uhuru wa nchi utakua na hali gani kama chombo kizito mfano wa jeshi la polisi kuendesha na wageni!
KWANI IGP WAO ALIKUWA MCHINA AU ASKARI WA KAWAIDA TU NDIYE ALIKUWA MCHINA BADO TUNAMIFUMO AMBAYA KWA DUNIA YA SASA HAINA FAIDA YOYOTE UKINIAMBIA KUAJIRI MCHINA TPDF WAWE WANAJESHI HAPO NITAKATAA
 
Hii inatokana na Viongozi wetu mafisadi kununuliwa
China mfungwa ni kama mtumwa, na biashara ya viungo vya binadamu imeshamiri sana. Wazungu wananunua sana maini ya binadamu kutoka China baada ya unywaji wa pombe uliopitiliza kuharibi maini yao. Waarabu ni figo kutokana na kisukari na magonjwa ya moyo ya muda mrefu. China inatuhumiwa kuuza viungo vya wafugwa kwa wateja kutoka nje. Hili pia limesababishwa na rushwa ya viongozi wetu wa Africa!
 
Teyari Wachina wameshaanza kuzengezengea ukiona ndege aina ya tai akizunguka angani sehemu fulani ujue chini kuna mnyama anakaribia kuwa mzoga.
Ni kweli. Zambia ni mfano, kuna taarifa kule wamejimilikisha ardhi kufidia madeni.
 
Shida kuu ya tza tumekosa uongozi bora vyote tunavyo. Tumekosa uongozi wenye weledi wa kutumia raslimali zetu kwa kuchochea uzalishaji wa ndani iwe ndo tegemeo na sio misaada ndo iwe tegemeo.
Tungewekeza kwenye kilimo tuilishe dunia tungepata pesa nyingi Sana.
V8 moja isiyo na tija kwa taifa ni sawa na trekta 6 brand new na vifaa vyake zingetumika kufukua ardhi zingezalisha ajira tele na kuleta pesa tele za kigeni Wala tusingehitaji mikopo
 
Mawazo haya mazuri yapite wapi katika nchi ya mihemuko ya siasa za kipumbavu, pole yetu
 
Hela yote iliyotumika kwenye SGR, ndege, Bwawa, kuuwa upinzani,nk Kama zingewekezwa kwenye kilimo zingesharudi Mara tatu. Na tusingehitaji mikopo.
. Fungua mipaka
.jenga viwanda vya zana za kilimo
.futa kabisa ushuru chochote kuhusu kilimo
.lima mazao yenye uhitaji Mkubwa duniani korosho, chikichi, alizeti, mtama, mahindi, mpunga, parachichi, katani, nk
.ongeza thamani mazao.
.
.
.
Tungepata pesa nyingi Sana za kigeni na tusingehitaji mikopo.
Tatizo la ajira lingetoweka.
 
1. Je SGR si ilikuwa ikijengwa na Waturuki? Tumevunja mkataba?
2. Bwawa la umeme ni Wamisri walikuwa wakijenga je tumevunja mkataba?
 
Hatuna jeuri mbele ya mabeberu. Cha muhimu ni Jiwe kutambua falsafa ya JK "ukitaka kula vya watu kubali kuliwa".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…