Serikali hongereni kwa kukwepa lawama ya uokoaji manusura wa Ajali ya Bukoba kupitia kupewa zawadi muokoaji Majaliwa

Serikali hongereni kwa kukwepa lawama ya uokoaji manusura wa Ajali ya Bukoba kupitia kupewa zawadi muokoaji Majaliwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Naona hivi sasa Watanzania (Waswahili) kama kawaida yao wameshahama katika Kuizungumzia Ajali na Mapungufu yake na sasa 97% ya Waswahili (Watanzania) wapo katika Kumzungumzia na Kumzawadia Muokoaji wa Taifa Dogo Majaliwa.

Taifa lenye Watu (Raia) makini kamwe hawawezi Kushadadia na Kufurahia Unafiki wa Kumpongeza na Kumzawadia Mtu (Muokoaji) Pesa na badala yake itajikita zaidi katika kupeana Elimu za Majanga na kujua Kiini cha Tatizo lililotokea na Kukemea kwa Nguvu moja Uzembe wa hali ya juu uliojitokeza.

Serikali yetu inajua mno Kutuhadaa.
 
Limeshakuwa suala la kitaifa sasa kumpongeza Majaliwa, ni sawa kwa vile ameonyesha ujasiri ambao hata baadhi ya askari hawanao.

Lakini pongezi kwake zisiondoe ukweli wa mapungufu ya vyombo vyetu katika uokozi. Nimekuwa najiuliza swali moja, hivi kwa mfano Ile crane iliyotumika leo kuitoa ndege ziwani ingetumika japo kuisogeza ndege ikiwa bado na wahanga ndani vifo vingekuwa 19 kweli.

Hivi kitengo cha maafa ambacho kiko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kazi yake kuu ni ipi, kungojea janga litokee wakatoe misaada ya mablangeti, vyakula n.k. Hivi vitengo husika vimejipanga vipi zinapotokea dharura kama hizi au ndio zinategemea uwepo wa wavuvi wenye zana duni kama kina Majaliwa?

Huko alikopelekwa Majaliwa kusomeshwa masuala ya uokozi hivi watajisikiaje kumfundisha mtu ambae bila mafunzo ameweza kusababisha uokozi wa watu 24 kitu ambacho wakufunzi wenyewe kwao ni ndoto, unamfundishaje ujasiri mtu wa hivyo.

Wakati tukiwa na majonzi ya kuwapoteza ndugu zetu 19 katika ajali hii, nadhani ni vema kama taifa, ajali hii iwe imetupa funzo la namna bora ya kujipanga ili majanga ya aina hii yakijitokeza tujue tunayakabili vipi. Hata kama hatunyosheani vidole basi na tujifunze kutokana na makosa.
 
Nilitegemea tu hili lazim lingetoke, ni kawaida kwa serikali yetu.
Hasa hasa ikijua kuwa inaongoza Watu wengi ( siyo Wote ) ambao ni 'Bogus' kabisa na hawana au hawajui pia kufanya 'Critical Thinking' ili Wajue mengi na Wajifunze.
 
Taifa la watu wa hovyo wambea wambea hawana uwezo wa ku-REASON.

Sasa hivi wanasambaza memes za kijana majaliwa wamesahau UZEMBE na UZUBAFU uliotokea

Watu kama hawa ni rahisi kuwatawala
 
Back
Top Bottom