Serikali huu ndio muda wa kuzibua na kujenga mitaro pamoja na kukarabati barabara mbovu, msisubiri mvua zifike muanze visingizio na maigizo

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Kila ikifika kipindi cha mvua ndio serikali huwa inashtuka kuanza kukarabati mitaro na njia na hapo ni baada ya kuwa mvua iliyoshinda siku mmoja imefanya mitaro ifurike na baadhi ya barabara kushindwa kufikika baada ya maji kujaa.

Pia soma: KERO - Shukran DAWASA kurekebisha palipokuwa na shida hadi kutengeneza shimo, TARURA lini mtakuja kuweka lami/zege maeneo ya Mbezi Beach kwa Dr. Hiza?

Kuna mdau humu huwa analeta shida za barabara ya Mbezi Beach mpaka anaanza kupewa ushari wa wananchi kufanya matengenezo wenyewe! Hii haikubaliki. Kodi mnazotukamua kila kukicha zinafanya kazi gani.

Siyo mnasubiri mvua zinaanza wananchi tunaanza kuhangaika njia hazipitiki ndio muanze kuja na visingizo vyenu mara tusubiri mvua ziishe, mara mitaro imejaa mchanga sijui nini na blaa blaa kibao.

Pia soma: Ni kwamba nchi ilikuwa na barabara nzuri muda wote mvua za El Nino ndio zimekuja kuharibu?

Tokeni maofisini huko ingieni mtaani kuona hali ikoje na kuanza ukarabati ukarabati na matengenezo mara moja.

Kuna malalamiko kibao ya wadau humu chukueni fanyieni kazi, ikifika kipindi cha mvua yaani unajuta na kuchukia kuishi Dar utafikiri tunaishi msituni. Kila mwenye wizara yake inayogusa maeneo haya toka huko ofisini ingia field hakikisha kazi zinafanyika.
 
Bora umekumbusha mapema,tusione rambirambi kwa sababu ya mafuriko ya kujitakia.
 
Back
Top Bottom