Serikali iache kuwaonea wafanyakazi, itafute vyanzo vingine vya mapato

Serikali iache kuwaonea wafanyakazi, itafute vyanzo vingine vya mapato

Halafu unalikuta jitu zima linakata kiuno huku likiimba "wataithoma nambaee...haha watanzania kuwatawala raha sana ndio maana wamefanywa mitaji na Chama mfu.
 
Mtumishi wa umma analipwa mshahara hapo hapo ananyang'anywa kupitia mikodi ya kizurumati, eti PAYE na makato mengine kibao kama bima ya afya na ongezeko la loan board ambalo wala hawakushirikishwa kwenye kuidhinisha, unashtukia tu unakatwa. Afadhali wafanyabiashara wana hata upenyo wa kukwepa hiyo mikodi ya kinyonyaji..lakini inakuwaje ukate kodi kwenye mishahara ya wafanyakazi wakati kila bidhaa na huduma wanayolipia inakatwa VAT!? nchi ngumu sana hii...
 
Muongo achana nae kodi kawaida kakopq mwenyewe hlsb asingekopa anepata 1.6M asingelalamika
Msipende kudanganya watu hapo makato ya kodi ni shs 536,541 tu. Fedha nyingine ni kwa faida ya mtumishi. Wasioelewa HESLB ni fedha aliyopewa mtumishi akiwa mwanafunzi kama asingekopa isingekatwa na wala sio watumishi wote wanaokatwa fedha hiyo. PSPF/NSSF ni akiba ya mtumishi atakapoacha kazi au kustaafu inatunzwa kwa faida yake ya baadae. Na Health Insurance ni fedha ya matibabu huitaji kulipia matibabu yako kutoka mfukoni hiyo ni bima ya matibabu. Halafu anaandika fedha inaenda serikalini bila aibu anasema inachukua nusu kwa nusu sio kweli toa tafsiri iliyosahihi kinachochukuliwa na serikali bila kurudiahwa ni 536,541 tu. TUWE WA KWELI

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom