Serikali iajiri walimu, watoto wanapoteza muda shuleni

Serikali iajiri walimu, watoto wanapoteza muda shuleni

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Kuna upungufu mkubwa wa walimu kwenye shule za umma
Nina mdogo wangu anasoma PCB huko Mwanza anasema haijawahi kumwona mwalimu wa Physics na Chemistry shuleni Toka mwezi wa 7

Mfano
Nilifika Wilaya ya Mkuranga shule msingi Koma ina mwalimu mmoja ambaye pia ndo mkuu wa shule.
Shule ya Msingi Kwale ina mwalimu mmoja pia.
Licha ya jitahada za uongozi wa vijiji na Kata kuomba walimu miaka nenda rudi

Kuna mwingine anasoma HGL- hawana walimu wa Geography na English Toka hiyo shule ianzishe advance

Wanasiasa tunakula watoto wenu wanasoma international schools na private schools hili haliwaumizi kichwa

Elimu Bure mnayotamba nayo ni hii ya shule kutokuwa na walimu, hamna maktaba, maabara, michezo.
Sasa hii ni elimu Bure au upuuzi tu

Hivi Kuna haja Gani ya kujenga mashule kama uyoga na hayana walimu,
Watoto wanaenda shule kufanya Nini, kucheza na kurudi nyumbani au kukua tu, hawapati maarifa

Walimu wapo wengi mtaani, hamtaki kuwapa kazi, mnangoja nini
Kama hamkujiandaa kwanini msifunge hizi shule?
 
Unajua nikisikiaga kuna shule ina mwalimu mmoja au zahanati ina muuguz mmoja yaan huwa siamin kabisa,inawezekanaje kwenye nchi ambayo taifa stars walipewa hela ya pongez karibia billion
 
Back
Top Bottom