DOKEZO Serikali iangalie kwa karibu zoezi la uandikishaji wanufaika wa TASAF Wilaya ya Serengeti

DOKEZO Serikali iangalie kwa karibu zoezi la uandikishaji wanufaika wa TASAF Wilaya ya Serengeti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

kiranja wa zamu2026

New Member
Joined
May 18, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Serikali inapaswa kuliangazia kwa karibu zoezi la uandikishaji wa wanufaika wa TASAF katika Kata ya Nyambureti, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, hususan katika vijiji vya Gusuhi, Nyambureti na Maburi.

Kuna madai ya kuwepo kwa udanganyifu mkubwa katika mchakato huo, jambo linalozua maswali kuhusu uwazi na uadilifu wa zoezi zima. Ikiwa madai haya yana ukweli, ni muhimu mamlaka husika zichukue hatua za haraka kufanya uchunguzi wa kina.

Pia, kuna umuhimu wa taasisi za uchunguzi, ikiwemo TAKUKURU, kuingilia kati ili kuchunguza tuhuma hizo na kubaini ukweli pamoja na kuwawajibisha wote watakaobainika kuhusika na vitendo vyovyote vinavyokiuka sheria na taratibu.
 
Back
Top Bottom