Serikali iangalie michezo ya kickboxing, anaweza kufa mtu uwanjani

Serikali iangalie michezo ya kickboxing, anaweza kufa mtu uwanjani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Aisee saa hizi Maulid Maulid amempiga mwenzake teke, jamaa kalala kwa zaidi ya dk 2, ameamka hajielewi kabisa hata wakati mshindi anatangazwa jamaa alishindwa kusimama.

Hii ni ligi nzuri napenda kuiangalia kwenye Vitasa plus, lakini nimeshangazwa hakuna Watu wa huduma ya kwanza uwanjani, maana jamaa walikuwa wanampepea kwa mashati, ameinuka hayuko vizuri wamemuacha aende mwenyewe nje.

Michezo tunaipenda ila ni muhimu serikali iweke sheria kali kama ulazima wa kuwepo kwa madaktari ulingoni, wapiganaji wawe na bima muda wanapokuwa ulingoni, otherwise kuna mtu atakufa na itakuwa too late.

Nawasilisha
 
Vitasa plus mzee baba
Jamaa amepigwa vibaya sana nimestuka kuona hakuna wataalamu wa afya, wanampepea na mashati. Jamaa kalala dk kibao, kainuka badi hajielewi na wamemuacha aende. Kesho tunaweza kusikia kafa, aligongwa mawashi moja mbaya sana
 
Ila kick boxing ni mchezo hatari kukiko hata boxing, ukiangalia majuu wanavyopigana unakuta watu wanaendelea kukabana chini kwa chini, mateke na ngumi halafu wengine wanaendelea kusafisha damu chini.

Kick 🥊 mchezo hatari sana
 
Ila kick boxing ni mchezo hatari kukiko hata boxing ,ukiangalia majuu wanavyopigana unakuta watu wanaendelea kukabana chini kwa chini ,mateke na ngumi halafu wengine wanaendelea kusafisha damu chini.

Kick 🥊 mchezo hatari sana
Hiyo sio kick boxing ni MMA - Mixed Martial Arsts, Kick boxing mtu hawezi kumfuata aliyeanguka
 
Kibaya zaidi ukute baada ya kuzinduka anampigia simu meneja wake ampe malipo yake hapokei simu.
 
Hii mambo ya kuiga iga tutakuja uana siku moja hata mimi kuna siku nililiona hili tatizo
 
Ipo siku yule Kidunda suleiman atakuja kumuua mtu halafu serikali ilaumiwe
 
Vigezo na Masharti kuzingatiwa..ni mchezo kama michezo mingine,watu wameshakufa wakicheza soka,basketball nk..
 
Aisee, mchezo wa ndondi ambao hautumii vifaa vya kujikinga uso na kufuata kanuni na masharti inavyotakiwa ni hatari sana. Inaweza kuleta matatizo ya mishipa na ubongo na madhara mengine kiafya.
 
hii michezo ya ngumi ilitakiwa izuiwe hapa nchini, ni hatari sana. Yani tamaa ya pesa inaweza kukuawa kimasihara tu
 
Back
Top Bottom