Kwitogelo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2023
- 310
- 442
Kuna huu utaratibu wa baadhi ya watu hasa askari wengi wanaochukua wanawake ambao siyo wapenzi wala wake zao na kwenda nao kujipima VVU kwa kutumia hivi vipimo vya rapid tests kabla ya kukutana nao kimwili lakini kitu kibaya zaidi hawa askari hawana elimu ya namna ya kuongea na mtu endapo atakutwa na maambukizi kitu kinachopelekea watu hao kushikwa na presha za ghafra na pengine kupoteza na maisha kabisa kutokana na kwamba hawa waathirika wanakuwa wanakosa ushauri wa kisaikolojia(psychological counselling).
Serikali iangalie namna ya kuwapatia hawa askari elimu ya namna ya kuongea na mtu atakaekutwa na VVU mara baada ya kujipima wenyewe kwasababu hakuna namna yoyote ile kwamba watu wasipimane au watumie mipira wakati vipimo vipo.