KERO Serikali iangalieni barabara kuu ya Arusha - Moshi. Vibao vingi vya kudhibiti mwendo na askari wengi wenye "tochi" ni kero

KERO Serikali iangalieni barabara kuu ya Arusha - Moshi. Vibao vingi vya kudhibiti mwendo na askari wengi wenye "tochi" ni kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Lukenya

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2024
Posts
640
Reaction score
811
Salaam!

Naomba kutoa hoja hii kuhusu barabara tajwa! Ina changamoto kubwa sana ya msongamano wa magari makubwa na madogo. Na hii inatokana na ufinyu wa barabara kutokana na mahitaji ya sasa. Tunaiomba serikali iangalie uwezekano wa kuikamilisha barabara hii kwa njia nne kuanzia ilipoishia eneo la Tengeru hadi njia panda ya Himo.

Lengo pia la hoja hii ni kutokana pia na umuhimu wa barabara barabara hii ktk sekta ya utalii ambayo inaiingizia serikali mapato mengi sana. Watalii wengi wanaotumia barabara hii kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwenda kupanda mlima K'njaro au kwenda mbuga za wanyama zilizopo ukanda wa kaskazini. Wanalalamikia wingi wa vibao vya speed limit (50kph) vilivyojaa njia nzima,ambavyo kiuhalisia vimewekwa kudhibiti mwendo kutokana na barabara hii kuwa jinsi ilivyo kwasasa kwa kuongezeka kwa makazi ya watu pembezoni mwa barabara.

Hali ambayo ingeweza kudhibitika kwa kuweka hizo njia 4 Kisha kuweka uzio katikati na kuijenga madaraja juu kwa ajili ya wavuka kwa miguu na kuruhusu magari kupita angalau kwa 80 kph speed. Hali ambayo itaokoa muda mwingi wa safari unaopotea kwa watumiaji wa barabara hii. Tuige kwa jirani zetu Kenya mfano wa barabara ya Thika super highway Kuna hadi 110kph na barabara imepita kwenye eneo la makazi ya watu. Tunatambua serikali Ina uwezo wa kutekeleza jambo hili kutokana na umuhimu wake.

Jambo lingine ni wingi wa traffic police na speed torch za kuvizia kwenye barabara hii. Jambo ambalo ninaamini ni kutokana na jinsi barabara hii kuwa jinsi ilivyo. Hivyo kulazimu kudhibiti mwendo wa magari Ili kupunguza ajali. Ila kama miundombinu hii ikiwekwa sawa kwa njia 4 na kuijenga madaraja ya juu, na vibao vya onyo kuzuiwa waenda kwa miguu kuhakikisha wanavuka kupitia madaraja yatakayojengwa kwa juu, hizo speed za 59 kph hazitakuwa na haja ya kuwepo.

Angalau serikali kupitia Tanroads waonyeshe weledi wao sasa kukabiliana na changamoto hizi zinazo dhibitika. Wageni wa nchi za nje wakipita na kuona hali hizi wanatucheka na kutudharau sana. Tunasafiri nao mara nyingi tunawasikia wakizungumza. Serikali amkeni tuijenge nchi yetu. Naomba kuwasilisha kwa wahusika waliopo humu wafikishe kwa viongozi wakuu.
 
Utamaduni wa hovyo sana tunao Watanzania. Haya mambo hayaombwi. Ni haki yetu na kama waliopo wameshindwa basi inabidi waondolewe kwa nguvu na kuwekwa wengine.

Nao wakishindwa wanaondelewa na kuwekwa wengine. Hivi ndivyo maendeleo yanavyopatikana na siyo kuomba!
 
Utamaduni wa hovyo sana tunao watanzania. Haya mambo hayaombwi. Ni haki yetu na kama waliopo wameshindwa basi inabidi waondolewe kwa nguvu na kuwekwa wengine. Nao wakishindwa wanaondelewa na kuwekwa wengine. Hivi ndivyo maendeleo yanavyopatikana na siyo kuomba!
Inalazimu kutumia njia hizi lengo likiwa ujumbe ufike. Maana watawala wetu ndicho wanachopenda.
 
Wakandarasi wetu kuna haja ya wao na washauri wa TANROAD na TARURA kuanza kuwekewa alama za miradi waliyosimamia na malalamiko iliopo.

Mfano hiyo ni barabara,imekamilika mji mpya Morogoro,magari ya mtaa hayaingii,na MORUWASA nao wameweka chemba ipo juu,gari zinapitaje?Shida ni wao wataalam.

PXL_20240809_145529985.MP.jpg
 
Barabara imepita mikoa miwili tofauti na majimbo tofauti yenye wabunge tofauti. Nimerahisisha kwa kulileta hapa Ili wahusika wafikishiwe au walione andiko hili. Na sio kwamba uliowataja hawalioni hili!
Kuna mkuu wa mkoa na mbunge ...
 
Ndiyo nakumbia kuwa hii njia haifanyi kazi. Hutakiwi kufanya kile watawala wanachopenda.
Shida kubwa sana ipo hapa. Tukiwakataa kwenye sanduku la kura ili tupate viongozi sahihi,wewe mwenyewe unafahamu kinachofanyika hadi matokeo yatangazwe. Tulisema tufuate haki ya kuandamana iliyoruhusiwa kikatiba unaambiwa majeshi yanafanya usafi kwa tar husika 😄😄. So what to do!? Ila ipo siku itakuwa kama unavyoeleza. Tutawalazimisha na sio kuwaomba.
 
Back
Top Bottom