Biohazard
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 2,197
- 1,465
Naomba tu nikufahamishe mito yetu tunatumia sana kwa boat ndogo nashangaa hufahamu hilo.Tanzania ina mito mingi tu lakini cha ajabu hatuitumii kwa usafiri kama mito mingi ya nchi za wenzetu zikiwemo jirani zetu Congo ambako watanzania waweza pia wekeza huko kwenye usafiri wa mito bado biashara ipo sana...
Mfano Mto Rufiji unaweza kutoka Selous Game Reserve hadi Bahari ya Hindi kwa boat na watu wanafanya routes hizo mara kazaa, Binafsi nimewahi toka Daraja la Mkapa kupitia Mto Rufiji mpaka Nyamisati Bahari ya Hindi kama utalii.
Unachokisema kinafanyika kwa utalii ila kwa usafiri wa umma ni ngumu sana kwa mito hii ya ndani ya bara isipokua maeneo ya pwani mengi wanasafiri kwa usafiri wa uma kwa kupitia mito mfano Wilaya ya Kibiti na Kilwa. Kuna watu wanishi Pombwe, Jaja, Kiasi nk wao usafiri wao ni mito tu na wana boat zao kabisa za abiria.
Kuna watu wanaishi Pande huko Kilwa pia wanatumia mto kutoka Kilwa Masoko kwenda Pande na nauli ni shs elfu 3 sijui wewe unamaanisha nini kusema mito inatiririka bure tu?