Serikali ianzishe kitengo cha Road Marshals ili kupunguza ajali za barabarani

Serikali ianzishe kitengo cha Road Marshals ili kupunguza ajali za barabarani

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Ajali za mabasi zimekuwa ni moja ya kilio kikubwa sana kwa wananchi na serikali kwa ujumla, taarifa kuhusu ajali za barabara ambazo zimepata kuwa ni sehemu ya kupoteza ndugu, rafiki na jamii zetu bado inaendelea kudhoofisha jamii. Ajali ya Mbeya ni moja ya ajali ambayo imeniumiza sana kiasi kwamba nimeona niandike wazo kuhusu moja ya suluhu kuhusu tatizo hili.
images (30).jpeg

Air Marshal kwa wengi wetu sio neno geni, labda kwa baadhi, ila hawa ni maafisa usalama ambao huwa kwenye ndege miongoni mwa abiria na hupewa maagizo maalumu ya kuzuia utekaji au suala lolote lenye kuleta uvunjifu wa amani ndani ya ndege ambazo huruka ndani ya anga la marekani.

Zaidi ya wasafiri milioni 2.9 ambao wanaingia na kutoka kwenye viwanja vya ndege ndani ya Marekani basi wanapata msaada mzuri wa Air Marshal ambao hujichanganya ndani ya abiria ndani ya ndege na wakiwa atayari kuzuia njama zozote za kigaidi na vitendo vya uhalifu.
images (31).jpeg

Air Marshals wamekuwa msaada mkubwa sana katika usalama wa abiria na usafiri wa anga ndani ya Marekani, na tokea mwaka 1961 maafisa hawa wameonesha weledi wa juu sana katika kuhakikisha matukio ya kigaidi au uhalifu hayatokei ndani ya ndege kadha wa kadha.

Rais George W. Bush ndo aliyeidhinisha upanuzi wa programu za Air Marshal ikiwa ni sehemu turufu ya Marekani katika kujilinda na kukabiliana na ugaidi. Idara ya usalama ya TSA imepata kuajiri zaidi ya maafisa maelfu ambao wana jukumu ya kuwaweka abiria salama katika safari nzima.​
images (32).jpeg

Nimeanzia mbali ili upate namna ambavyo TSA inafanya kazi na mamlaka ya usafiri wa anga katika kuhakikisha abiria wanakuwa salama salimini kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa safari. Binafsi hii ni moja ya sehemu ambayo mamlaka za usalama zinaweza kutumia kwa ushirikiano na LATRA katika kuzuia matukio ya ujambazi wakati mabasi yakiwa kwenye safari zake pamoja na kuzuia ajari ambazo baadhi ya ajali hizi vyanzo vyake ni madereva kwa kiasi chake.

Chukulia picha umepanda zako Scandinavia na unatoka Dar es Salaam kuelekea Shinyanga, mnatoka Dar es Salaam salama na kuanza kuitafuta Morogoro ila ghafla kunatokea sitofahamu na dereva anaanza kuendesha basi lenu kama yupo kwenye filamu ya Fast & Furious, dereva anajiona Vin Diesel. Anatokea mtu mmoja na kujitambulisha kuwa yeye ni Road Marshal na yupo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mpo salama katika safari yenu, na dakika tano baadaye defender inafika eneo ambalo basi lenu lipo na kumtia nguvuni dereva.
images (33).jpeg

Road Marshal wanaweza kuwa msaada mkubwa sana katika kusaidia kupunguza vitu kama, ajali za barabarani, wizi wa vitu ndani ya mabasi (Road Marshal atakuwa mtu wa kwanza kuingia kwenye basi na mtu wa mwisho ambapo atahakikisha kuwa kila abiria amefika kwenye kituo husika kulingana na tiketi yake), Road Marshal watakuwa ni sehemu bora sana ya kutoa taarifa kuhusu utendaji kazi wa dereva husika, na atakuwa akitoa report yake pindi tu wakiingia stendi pamoja na kusimama kwa ajili ya kuchimba dawa (kujisaidia).

Road Marshal wawe ni kikosi maalumu cha maafisa ambacho kitafanya kazi kwa ukaribu sana na Polisi pamoja na Traffic kwa kiasi kikubwa endapo kukiwa na uvunjifu wa sheria basi RM wawe watu wa kulifahamu na kutoa taarifa kwa wepesi zaidi katika mamlaka, taarifa za number plate, pamoja na idadi ya abiria. Na pindi basi husika likiingia stendi basi kama dereva amehusika kwenye kuvunja sheria au kuleta hofu katika uendeshaji wake, polisi watachukua hatua zao na abiria waendelee na safari.​
images (34).jpeg

Kwa wale wanaofanya safari kutoka jiji kwenda jiji basi wawepo Road Marshal ambao watakuwa ni Special Road Marshal ama Senior Road Marshal, mfano Basi B kutoka Dar es Salaam likifanya safari kwenda Mwanza ndani yake kuna kuwa na Special Road Marshal, Kama basi M linatoka Mwanza kueleka Iringa basi ndani yake kutakuwepo na Road Marshal wa kawaida tu. Hii itaonesha utofauti katika utendaji wa kazi kwani tunategemea Special Road Marshal ambao ni Seniors kuwa na uwezo mkubwa na kuliko wa Road Marshal wa kawaida.
Namna ya kuwapata Road Marshal:

Ushirikiano baina ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Wizara ya Mambo ya ndani ishirikiane na majeshi, JWTZ, JKT, Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokozi katika kutoa mafunzo ya kwa vijana ambao watakuwa tayari kimwili na kiakili kufanya kazi ya Road Marshal sehemu yoyote ambayo watapangiwa.​
images (36).jpeg

Vijana wafundishe mbinu za uokozi na usalama, wawe vijana wenye utashi na sio wale wenye D mbili, na masomo yasiyo ya dini, bali wawe ni watu wenye utimamu mkubwa wa akili na mwili kiasi kwamba anaweza kubadilisha haiba yake kwa muda mchache kuendana na tukio fulani.

Ushirikiano baina ya Wizara ya Mambo ya ndani, Wizara ya Uchukuzi pamoja na Wizara ya Afya pamoja na taasisi zilizopo chini yao:

Wizara hizi tatu zishirikiane katika kutoka mafunzo bora ya udereva kwa vijana hawa endapo kama kukitokea tatizo njiani basi Road Marshal aweze kutoa msaada kwa muda mfupi. Wizara ya Uchukuzi kupitia Chuo cha NIT inaweza kutoa mafunzo maalumu kwa hawa Road Marshal namna ya kuendesha magari haswa nyakati za dharura, mfano wakati wa wahalifu wameweka mawe na vizuizi katikati ya barabara.​
images (35).jpeg

Pia Wizara ya Afya ipate kuwafundisha RM namna ya kutoa huduma za kwanza kwa abiria pamoja na namna ya kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa abiria endapo kukitokea tatizo lolote barabara, kwani kuna wengine wamekuwa wakisafirisha watu wasio raia wa Tanzania (sioni vyema kama nikisema wakimbizi) lakini kuna wengine hubeba na kusafirisha madawa ya kulevya, pia RM wanaweza kufundishwa namna ya kuzungumza na abiria na kufahamiana na kufahamu kama kuna hatari ndani au nje ya chombo husika cha usafiri (kufahamu saikolojia zao).​
images (37).jpeg

Nina imani tukiwa na Road Marshals katika mabasi yetu itapunguza kwa kiasi kikubwa masuala ya ajali haswa zile ambazo vyanzo vyake ni uzembe wa madereva au matatizo yanayoepukika. Lakini pia hii itakuwa ni fursa kwa vijana wa kitanzania ambao wanatamani kuwa maafisa usalama kwani itawafungulia njia kuingia kwenye ajira ndani ya majeshi yetu huku wakihusika na huduma za jamii moja kwa moja.​
images (30).jpeg

Angalizo: Mamlaka msitumie maafisa RM kama daraja la kuteka watu bila utaratibu au kutoa taarifa kuwa watu fulani wapo ndani ya basi fulani hivyo wanapaswa kukamatwa, bali wawe daraja baina ya LATRA, vyombo vya usalama pamoja na jamii katika kuepusha ajali pamoja na uhalifu.

NB: Nimetumia neno Road Marshals sio kwa nia mbaya bali ni kwa nia ya kuonesha maafisa usalama ambao watakuwa na raia katika safari.
 
Jinamizi la ajali za barabarani linaloendelea kuitafuna kila siku Tanzania na kuwaacha wananchi wake kwenye misiba, majonzi, na simanzi zisizoisha limenifanya nitakari kwa muda juu ya ni nini haswa huwa kinawasukuma waliokabidhiwa ofisi za umma kufanya maamuzi yanayohusu maisha, uhai, usalama, na ustawi wa wananchi.​
 
Ndugu una kitu ila sasa si ajabu hao road marshall waka wala rushwa badala ya traffic
Ndo tatizo kubwa la nchi yetu ila hawa ndo wangesaidia kuzuia ajali mapema sana
 
"Ajali za barabarani husababisha karibu vifo milioni 1.19 duniani kote kila mwaka. Mwaka 2021, asilimia 92 ya vifo vya barabarani vilitokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati" kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa
 
Back
Top Bottom