Yaani mnacho shauri huwa mna exclude Halmashauri, utafikiri Halmashauri siyo sehemu ya Serikali.
Tatizo kubwa la nchi hii, hakuna Muunganiko.
Serikali Kuu na taasisi zake inajipendelea kwenye kila kitu (nadhani isipokuwa Maafisa Tarafa) wanaofanya kazi chini ya DC.
Watumishi unaowasema waote wanaweza kupatikana chini ya Halmashauri.
Halmashauri zinaendeshwa Kama watu hawakwenda shule.
Ziko zig zag, Kwasababu serikali inathamini zaidi watu wanaoifadisha na siyo watu wanaofaidisha jamii.
Yaani wewe Mhasibu unayehudumia watu 3,000 huko TAMISEMI huna maana, ila Mhasibu mwenye elimu kama wewe huko TRA anaishi ulimwengu mwingine kabisa.
Shida kubwa kwa sheria za fedha za nchi hii.
- Halmashauri zinakaa zinatunga
- Serikali kuu (Mof) inakaa inatunga sheria
- Taasisi (TMDA, TBS, TMDA,NEMC, Bodi ya Nyama, Bodi ya KOROSHO, Bodi ya Pamba, Bodi ya Kahawa, Ufuta nk) wanakaa wanatunga sheria.
Hawa wote kila mmoja anakaa anatunga kwa wakati wake, bila kumhusisha mwenzake na TARGET ni mtu MMOJA yule yule. Lazima aumie.
Suluhisho kubwa 2:
- Kuwekwe utaratibu (mmoja) suala lolote linalohusu kukusanya mapato kutoka kwa mtu litokee sehemu moja, ili kuepeuka kukomaa na mtu kwa Kodi 1,000 bila kujia.
- Kuongeza wigo wa Kodi ( hii itapunguza ukubwa wa Kodi, kwa mtu mmoja mmoja).