Serikali ianzishe "Maafisa Kodi wa Kata" na TRA ianzishe "mawakala" wa TRA

Kingine kinachokera ni pale unapolipia kila kitu ukaenda TRA kupata huduma wanaaza upya kukudai ulicholipia mwaka jana au miezi 2 iliyolipa usipoonyesha vielelezo/slip kuwa umeishalipa wanakutwanga kodi nyingine, ni wasumbufu kupita kiasi, sijui computer zao hazitunzi kumbukumbu, wanakera mpaka basi.
 
Pale kariakoo sijaona bango linalowataka watuhumiwa wa CAG washughulikiwe, make wamekula kodi zetu.
 
Hapo tunazidi kuongeza rundo la walamba asali na Wala rushwa
 
Dah mzigo mmoja kodi 3 bado hujaufikisha dukani
 
Clear
Wale wanaouza efd machines?
Wapo kila mtaa au ndo uwafate pembeni ya Tra?
Wanamaliza kazi zote au zingine uende tra?
Mawakala wa bank unamaliza nao kila kitu mtaani...hufiki bank
Cliaring Agent ni Mawakala wa forodha, tunamakampini zaidi ya 1,000 na kazi yao ni kusaidia wafanya biashara kulipa kodi na kuwaelimisha, kumbuka wanasema chuo cha kodi cha TRA so wanautaalamu wa kodi mazuri tu
 
Watauana
 
Kuuliza si ujinga, hivi forodha ni nini sijawahi kulielewa hili neno, msaada tafadhali
 
Shida siyo kwamba computer zimeacha kutunza kumbukumbu tatizo hapa ni kwamba hao wacanyakazi ww TRA na ambao ndo wenye access na hizo computer hawataki kujituma kwa maana ya kutafuta kodi halali kutoka mwenye vyanzo vipya vya mapato hapa kwa sababu wanakufahamu wewe wanataka kurahisi kazi yao ukusanyaji kodi kwamba wakusanye tu ili kufikia lengo ama target ya ukusanyaji waliyopewa.

kwa hiyo wanachokifanya hapa ni ubabaishaji wakifahamu kabisa kwamba pengine wafanyabiashara wanaweza kuwa hawajatunza kumbukumbu za malipo ama wamepoteza kumbukumbu unapokosa unakuwa umenasa kwenye 18 zao kwamba wanakuchapa kodi bila huruma kwa sababu tu huwezi ingia kwenye computer zao na kufungua mfumo ili uone rekodi yako ya malipo uliyofanya siku za nyuma.

kwenye computer zao taarifa zako zote zipo kwenye faili lako bora tu wanayo TIN ama vat registration.namba yako .
 
Ni vema kulipa Kodi kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake lakini kwa tabia ya matumizi ya hovyo ya pesa ya umma na ufisadi unao ibuliwa kila mwaka na CAG nakushauri kwepa Kodi utakuja kunishukuru baadaye
 
Ni wajinga sana, sijui hii tabia itakoma lini.
 
[emoji2956][emoji2956]
 
Wale wanaouza efd machines?
Wapo kila mtaa au ndo uwafate pembeni ya Tra?
Wanamaliza kazi zote au zingine uende tra?
Mawakala wa bank unamaliza nao kila kitu mtaani...hufiki bank
Kwani tatizo kubwa na sugu ni nini?

  • Kodi nyingi na kubwa kwa mtu mmoja
  • Elimu ya Kodi
  • Ugumu katika kulipa Kodi
  • Watumishi wachache TRA au
  • TRA Kukosa wafanyakazi ngazi ya chini?

Kwasababu naona mapendekezo yako, hayatatui tatizo.

Mfano: Kariakoo ni mkoa maalum wa Kikodi kwa TRA maana yake ima huduma zote za TRA zinazojitegemea.

Sasa Kama wao KARIAKOO Wana mgogoro mkubwa na TRA, na wana watumishi wengi wa TRA wanaofanya kazi eneo Hilo PEKEE. Huyo TRA kata mmoja ndio ataweza KUWA MWISHO WA MATATIZO??
 
Ndio maana tunataka Katiba Mpya.

1. Tanzania ina utitiri wa kodi kwa sababu ina utitiri wa taasisi na mamlaka na kila moja inataka kodi/ushuru/tozo kujiendesha.
Zaidi ya 35% ya taasisi serikali zinafanya kazi zenye kudurufiana (duplication).

2. Muundo wa serikali pia ni tatizo na mzigo mkubwa kwa mlipa kodi. Kwa mfano, kwenye ngazi ya Wilaya una hawa viongozi/mamlaka:-
a. Mkuu wa Wilaya
b. Mkurugenzi wa Halmashauri/Jiji
c. Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri
d. Mbunge
Hao wawili wa mwanzo ni wateuliwa wa Rais, wana mamlaka zao, wana bajeti na mafungu yao (separately) - wana watumishi wao, majengo, magari nk

3. Kwa upande wa TRA (Wizara ya Fedha) Viwango vya kodi (tax rates) zaidi ya 40% ni vikubwa na sio rafiki.
Hivyo kusababisha ukwepaji kodi, rushwa nk nk
Waweke Viwango vya kati rafiki na kuongeza elimu ya kodi nk

4. Ubadhirifu na usimamizi mbovu wa fedha za umma - ikiwemo wizi na ufisadi.
Hili nalo, kama #3 hapo juu; linapunguza ari na ulipaji kodi wa hiari - "kwamba si zitaliwa tu"

Katiba mpya itatuwezesha kurudi kwenye drawing board, kupanga upya muundo wa serikali, kuweka uwaazi na uwajibikaji katika namna ambayo matatizo kama haya yatapungua kiasi kikubwa
 
Matatizo ni mengi mno nchi mzima ccm watolewe kwanguvu waje watu wengine hawa ndio chanzo cha matatizo yote. Hata ufanyeje nikazi bure.
 
☑️
 
Tatizo la Tanzania walipa kodi ni wachache huku wengi wakifichwa kwenye kivuli cha wanyonge.

Siasa nyingi sana, CCM wakisema watoze kodi, Wapinzani wanasema Wanyonge wanaonewa, na kinyume chake.

Ili nchi iendelee yatakiwa TRA iwe huru, isifungwe na wanasiasa.

Mawakala ni chanzo cha rushwa.

Halamshauri hutoa leseni baada ya kupata Tax Clearance.

Halmashauri zatakiwa ziongeze nguvu ya kuzunguka mitaani kwa kupitia Serikali za Mitaa ili zieze himiza ukataji wa leseni, na ili upewe leseni lazima upite TRA.

Tukiachana Siasa na utetezi wa kipumbavu kodi itakuwa ndogo, vinginevyo tukomea kiendelea tozwa kodi kubwa kwenye huduma ie mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…