A
Anonymous
Guest
Sisi Wananchi wa Kata ya vijibweni, Mtaa ya Kibene na nyingine zilizopo jirani na maeneo hayo (Dar es Salaam), kumekuwepo na matukio ya kuogofya na yanayotokea mfululizo ikiwemo kuokotwa kwa miili ya watu.
Siku za hivi karibuni miili zaidi ya mitatu imekutwa kwenye eneo hilo kwa nyakati tofauti jambo ambalo linatufanya tuwe na hofu muda wote kuhusu maisha yetu.
Eneo hilo kwa sasa kumekuwa na matukio pia ya ubakaji na uporaji ambayo yanaacha majeraha na makovu kwa baadhi ya waathirika.
Tetesi zilizopo ni kuwa eneo hilo ni mali ya Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) japokuwa hakuna uhakika wa hilo kwa kuwa hakuna wamiliki au mmiliki ambaye amejitokeza kuweka wazi juu ya umiliki na taarifa zilizopo ni kuwa hakuna Mwananchi anayeruhusiwa kuliendeleza kwa namna yoyote.
Hali hiyo imesababisha Wanafunzi kuwa katika mazingira ya hatari wakati wakitumia barabara iliyopo katikati ya msitu huo kwenda na kurudi kutoka shuleni.
Moja kati ya matukio ambayo nimeshashuhudia ni baadhi ya Wanafunzi kuporwa vitu vyao ikiwemo mabegi ya shule na wakati mwingine kutakiwa kutoa pesa walizonazo hata kama ni kidogo.
Kinachotusikitisha zaidi ni kuwa licha ya kutoa taarifa Polisi tunapokuta miili katika pori hilo, Jeshi la Polisi limekuwa likifika, linachukua miili na kuondoka naye bila kuweka wazi kinachoendelea, hawatuambii chochote sisi Wananchi tunaotoa taarifa kwao na tunaoishi maeneo hayo.
Wananchi wakishuhudia mwili uliotupwa katika Pori hilo.
Natoa wito kwa Serikali, kwanza iwekwe wazi kuwa eneo huli linamilikiwa na nani? Kwanini hawataki tuliendeleze? Uhalifu unaoendelea nini hatma yake? Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya usalama vimeshindwa kudhibiti uhalifu unaendelea?
Kumekuwa na taarifa kuwa miili inayookotwa ni kutoka kwa watu wa maeneo mengine mbali na hapa, inavyoonekana baada ya uhalifu kufanyika imekuwa ikija kutupwa huku.
Tunaomba kilio hiki kisikike na kimfikie hadia Rais Samia Suluhu Hassan ajue kuwa Wananchi wake wanauliwa, wanatateseka na wanaishi kwa hofu.
====== =====
Machi 16, 2024, Jeshi la Polisi Kata ya Vijibweni, kupitia Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP), Angelo, Polisi Kata ya Kisiwani, (A/INSP) Mintanga pamoja na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Kigamboni, (A/INSP) Getruda walifanya walifanya kikao na wananchi wa maeneo hayo kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.