KERO Serikali ichunguze na kuchukua hatua wanachofanyiwa Wazawa katika Kampuni za ujenzi/barabara/majengo n.k

KERO Serikali ichunguze na kuchukua hatua wanachofanyiwa Wazawa katika Kampuni za ujenzi/barabara/majengo n.k

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ninaomba mamlaka husika ziangalie kero za Wafanyakazi kwenye baadhi ya kampuni za ujenzi wa barabara nchini. Mimi ni mmoja wa wafanyakazi kwenye kampuni ya ujenzi wa barabara na tunakutana na changamoto zifuatazo:

1. Kufanyishwa kazi nje ya muda uliopangwa kisheria bila kulipwa malipo ya muda wa ziada (overtime).

2. Kufanyishwa kazi bila kuwekewa michango ya hifadhi ya jamii kama National Social Security Fund (NSSF), jambo ambalo ni kinyume na sheria za kazi.

3. Wafanyakazi wengi hatuna mikataba ya kazi, na hata pale mfanyakazi anapoumia kazini hapati msaada au fidia inayostahili.

4. Kima cha chini,cha malipo kwa siku awazingatii wanalipa wanavyo taka wao

5. Awalipi Kodi mbalimbali ikiwemo kodi iliyo takiwa kukatwa ktk mshaara wa wafanyakazi

Pia naomba mamlaka zinazosimamia wakandarasi wa barabara kama Tanzania Rural and Urban Roads Agency ( TARURA ) na Tanzania National Roads Agency (TANROADS) ziongeze ufuatiliaji wa hali za wafanyakazi kwenye miradi ya barabara. Ni muhimu kujua wafanyakazi wanalipwa vipi, wana mikataba au la, na kama wanapatiwa haki zao kwa mujibu wa sheria za kazi za Tanzania.

Tunaomba mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Kazi zichukue hatua ili kulinda haki na ustawi wa wafanyakazi.
 
Back
Top Bottom