Serikali idhibiti mahindi kwenda nje

Serikali idhibiti mahindi kwenda nje

Hivi unajua chain of supply (value chain) ?
Kwa taarifa yako mwaka huu bonde letu la kilombero wakulima tumenufaika Sana kuliko miaka miwili ya nyuma . Acheni tupate faida mbona miaka ya nyuma Bei ilivyoshuka wakulima tulipambana wenyewe ? Wenzetu mlibaki kimya kwanini hamkutusemea?
Sasa kwani mie nimepinga nini hapo?

Mie si nimeeleza uhalisia wanaonufaika zaidi ni hao watu wa kati hapo
 
Mkuu madalali na walanguzi wa mazao wanaojiita wakulima watakuja sasa hivi kukutolea povu na kukuuliza maswali kama na wewe umelima.....

Dalali bei kuwa chini au kuwa juu yeye inamdhuru vipi? Huyo mlanguzi mahindi yakiwa chini si ndio anayanunua anayasubiria yapande?

Msipende kudandia migongo ya wakulima wa Mahindi kila siku maana hata hayo mahindi wakulima wake wengi wao ni masikini
 
Ifahamike kuwa mahindi yanaenda kenya ila wakulima hawanufaiki kivile, wanaonufaika ni wafanyabiashara wanaozukuka na magari kununua mahindi kwa bei rahisi na kuyauza ghali.

Dunia ya leo Kuna bei za kilaliaji kwenye mazao pamoja Na kuenea Kwa Internet na mitandao ya simu?

Hilo gunia unalinunua sh ngapi na unakoenda kuuza unaenda kuuza sh ngapi?
 
Huyu mama asipotumia akili ya kawaida ya binadamu Watanzania kwa mara ya kwanza tutakufa kwa njaa. Tumemsikia Waziri wake Bashe akithibitisha kuwa mipaka haitofungwa kwa biashara ya nafaka hasa mahindi na mchele. Baya zaidi wafanyabiashara toka nchi za jirani wanakwenda hadi vijijini kwa wa kulima kununua mazao. Jambo ambao ni kinyume cha kanuni tulizojiwekea kwa tawala zilizopita. Mama amka Waziri wako kwa hili anafanya makosa yatakayo kugharimu 2025 si mbali.
Kwa tume ipi ya Uchaguzi?
 
nayaona malori ya kenya yanapishana kuzoa mahindi wakati sado tunauziwa 4500, sema dua la kuku halimpati mwewe.

maisha ni magumu kwa watu wa hali ya chini
Watu wa hali ya chini nchi hii ni wakulima, acheni wauze mahindi yao kwa mnunuzi anayewapa bei nzuri
 
Maisha ni kutegemeana, wote hatuwezi kuwa wakulima, ndio maana unasikia watu wanalalamika bei za mafuta, mazao,vifaa vya ujenzi n.k.

Bidhaa moja ikipanda inaathiri nyingine.
Kila mtu ashinde mechi zake..ni watu gani wanaopangiwa wateja wa kuwauzia bidhaa zao hapa nchni kasoro wakulima pekee?
 
Mkuu madalali na walanguzi wa mazao wanaojiita wakulima watakuja sasa hivi kukutolea povu na kukuuliza maswali kama na wewe umelima.....
Na bado Kampala inategemea kulishwa mchele na Kahama,Ifakara na mpanda.

Wakulima kama wangekuwa ndio wauzaji wa moja kwa moja wangenufaika sana na mazao yao bahati mbaya madalali na wafanyabiashara ndio wanufaika wa hali ya sasa.
Kila soko lina wazalishaji, madalali na wafanyabishara wa kati kisha ndio mnunuzi, kuanzia kwenye madini, nyumba, mashamba, vifaa vya ujenzi, vyakula n.k ndio uchumi ulivyo
 
Maslai ya watanzania yako kwenye chakula ilo ata serikal inalijua haina haja ya kuwapa ushauri

Mtanzania akikosa msosi utaona uzuri na ubaya wake na ata mapinduzi wanayongelea kla sku wanasiasa yatawezeka sku watanzania wakikosa ugari
Ukimwambia Mtz suala la mafuta, sjui bei za bando wala hawakuelew ila subili mahindi yapande bei uzi km izi zinakua ming sana
Aliyefanya kazi na asile, na asipokula afe-Magufuli
 
Huyu mama asipotumia akili ya kawaida ya binadamu Watanzania kwa mara ya kwanza tutakufa kwa njaa. Tumemsikia Waziri wake Bashe akithibitisha kuwa mipaka haitofungwa kwa biashara ya nafaka hasa mahindi na mchele. Baya zaidi wafanyabiashara toka nchi za jirani wanakwenda hadi vijijini kwa wa kulima kununua mazao. Jambo ambao ni kinyume cha kanuni tulizojiwekea kwa tawala zilizopita. Mama amka Waziri wako kwa hili anafanya makosa yatakayo kugharimu 2025 si mbali.
Magufuli alisema asiyefanya kazi na asile, na asipokula acha afe, acha wakulima wapate hela waheshimike na wao
 
Huyu mama asipotumia akili ya kawaida ya binadamu Watanzania kwa mara ya kwanza tutakufa kwa njaa. Tumemsikia Waziri wake Bashe akithibitisha kuwa mipaka haitofungwa kwa biashara ya nafaka hasa mahindi na mchele. Baya zaidi wafanyabiashara toka nchi za jirani wanakwenda hadi vijijini kwa wa kulima kununua mazao. Jambo ambao ni kinyume cha kanuni tulizojiwekea kwa tawala zilizopita. Mama amka Waziri wako kwa hili anafanya makosa yatakayo kugharimu 2025 si mbali.
Wavivu ndio watakufa kwa njaa mambo ya kupenda mbeleko kupitia jasho la wakulima

Mkulima hasaidiwi kwenye kulima ila mnataka apangiwe wa kumuuzia na bei atayouza
 
Back
Top Bottom