Serikali idhibiti mahindi kwenda nje

Sasa kwani mie nimepinga nini hapo?

Mie si nimeeleza uhalisia wanaonufaika zaidi ni hao watu wa kati hapo
 
nayaona malori ya kenya yanapishana kuzoa mahindi wakati sado tunauziwa 4500, sema dua la kuku halimpati mwewe.

maisha ni magumu kwa watu wa hali ya chini


Hao hao wa hali ya chini ndio wanaolima Mahindi hayo
 
Mkuu madalali na walanguzi wa mazao wanaojiita wakulima watakuja sasa hivi kukutolea povu na kukuuliza maswali kama na wewe umelima.....

Dalali bei kuwa chini au kuwa juu yeye inamdhuru vipi? Huyo mlanguzi mahindi yakiwa chini si ndio anayanunua anayasubiria yapande?

Msipende kudandia migongo ya wakulima wa Mahindi kila siku maana hata hayo mahindi wakulima wake wengi wao ni masikini
 
Ifahamike kuwa mahindi yanaenda kenya ila wakulima hawanufaiki kivile, wanaonufaika ni wafanyabiashara wanaozukuka na magari kununua mahindi kwa bei rahisi na kuyauza ghali.

Dunia ya leo Kuna bei za kilaliaji kwenye mazao pamoja Na kuenea Kwa Internet na mitandao ya simu?

Hilo gunia unalinunua sh ngapi na unakoenda kuuza unaenda kuuza sh ngapi?
 
Kwa tume ipi ya Uchaguzi?
 
nayaona malori ya kenya yanapishana kuzoa mahindi wakati sado tunauziwa 4500, sema dua la kuku halimpati mwewe.

maisha ni magumu kwa watu wa hali ya chini
Watu wa hali ya chini nchi hii ni wakulima, acheni wauze mahindi yao kwa mnunuzi anayewapa bei nzuri
 
Maisha ni kutegemeana, wote hatuwezi kuwa wakulima, ndio maana unasikia watu wanalalamika bei za mafuta, mazao,vifaa vya ujenzi n.k.

Bidhaa moja ikipanda inaathiri nyingine.
Kila mtu ashinde mechi zake..ni watu gani wanaopangiwa wateja wa kuwauzia bidhaa zao hapa nchni kasoro wakulima pekee?
 
Mkuu madalali na walanguzi wa mazao wanaojiita wakulima watakuja sasa hivi kukutolea povu na kukuuliza maswali kama na wewe umelima.....
Na bado Kampala inategemea kulishwa mchele na Kahama,Ifakara na mpanda.

Wakulima kama wangekuwa ndio wauzaji wa moja kwa moja wangenufaika sana na mazao yao bahati mbaya madalali na wafanyabiashara ndio wanufaika wa hali ya sasa.
Kila soko lina wazalishaji, madalali na wafanyabishara wa kati kisha ndio mnunuzi, kuanzia kwenye madini, nyumba, mashamba, vifaa vya ujenzi, vyakula n.k ndio uchumi ulivyo
 
Bei ya mhindi huko Arusha vijijini haishikiki. Serikali kupitia Waziri wake Bashe ithibiti mahindi kwenda nje

Watu wataumia na ukosefu wa mahindi

Sio mahindi tu, na hata mchele na maharagwe yazuiwe kutoka.
 
Aliyefanya kazi na asile, na asipokula afe-Magufuli
 
Magufuli alisema asiyefanya kazi na asile, na asipokula acha afe, acha wakulima wapate hela waheshimike na wao
 
Wavivu ndio watakufa kwa njaa mambo ya kupenda mbeleko kupitia jasho la wakulima

Mkulima hasaidiwi kwenye kulima ila mnataka apangiwe wa kumuuzia na bei atayouza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…