Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
Ni siku chache tangu hospitali ya Muhimbili Orthopedic Institute (MOI) kutoa habari njema juu ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo baada ya kupatwa na ajali ya kugongwa na basi la Mwendokasi. Kiukweli ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu ameendelea kumuweka hai na salama mpaka leo hii kwani ajali ilikuwa ni yenye kuogofya.
Lakini, nilitamani sana mgonjwa huyu_hali yake itakapotengemaa basi serikali yetu pendwa ichukue jukumu la kumpatia support zaidi katika kuhakikisha anaendelea kuishi katika mazingira mazuri kwani.
Pindi atakapopata ahueni bado kuna changamoto nyingi ambazo zitaendelea kumkabili mfano, anaweza pata msongo wa mawazo (Depression) pia tatizo la kumbukumbu ya ajali (Post Traumatic Stress Disorder) n.k. hivyo anahitaji mazingira rafiki ili kumjenga upya kifikra, mawazo na hata mitazamo.
NB: Ni mawazo tu ndugu zangu wa JamiiForums