Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ishirikiane na TFF na bodi zote na taasisi zinazohusika kuutafutia matumizi ya dharula uwanja wa Zanzibar hili Mechi ipigwe Lupaso kwa maana ya uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kwanza Simba imeuzoea sana uwanja wa Benjaminj Mkapa kiasi kwamba wanajua kuutumia vizuri kujinufaisha kimatokeo. Pili uwanja wa Mkapa huko katikati ya jiji la Dar es Salaam, unafikika kirahisi na watu wa Mikoani na watu wa visiwani zanzibar tofauti na Uwanja wa Zanzibar ambao ni mpaka watu wavuke maji kwenda kutizama kabumbu. Kama ni kweli Mechi inatakiwa ipate mashabiki wengi basi Lupaso ndio uwanja pekee hapa Tanzania unaoweza kufanya fainali iwe ya kihistoria.
Tunajua timu ya Berkane tayari wapo kwenye wasiwasi wa kuutumia uwanja wa Mkapa kwa vigezo kuwa Simba uwa ni Timu hatari sana ikiwa pale Lupaso hivyo wanalazimika kutumia kila mbinu kulazimisha uwanja wa Zanzibar ndio utumike, jambo ambalo halikubaliki. Sisi ndio tuamue Simba icheze wapi kwa kuwasilisha viwanja vyenye ubora unaohitajika na Mkapa tayari imekidhi vigezo hivyo kwa kufanyiwa ukarabat wa hali ya kiwango cha juu (Wasukuma wanasema kiwango cha lami)
Hivyo basi sisi kama wanalunyasi, wanamsimbazi, wekundi wa msimbazi tunaomba Mechi ipigwe Mkapa iwe kwa namna yoyote na uwanja wa Zanzibar utafutiwe sababu yeyote ya Dharula hili husitumike. Utafutiwe shughuli ya maana ikiwezekama mwezi mzima, apelekwe hata Mwaposa akeshe hapo mwezi mzima. Hii inawezekana kwa sababu mpira sio uwanjani tu, ushindi utafutwa toka nje ya uwanja.