Serikali ifanye nini ili uchumi wetu uipiku Kenya na mataifa yenye uchumi mkubwa kuliko sisi?

Kufuatana na tafiti za kitaalam, CCM imejaa watu wajinga. Unategemea mjinga akuongoze kuelekea kwenye maendeleo?

Chini ya uongozi wa CCM, hayo unayoyafikiria sahau. Tutaendelea kuwa mikia.
 
Upo sahihi sana mkuu,hili swali lako ni paper kabisa linatakiwa lifanyiwe utafiti kabisa na wataalam ili waje na ufumbuzi wake mantashallah
 
Rasilimali zote hazina maana kama usipokuwa na uongozi wenye uwezo. Kwa sasa, nakadiria zaidi ya 80% viongozi wote, wana akili chini ya kiwango cha akili ya kawaida.

Tumebarikiwa kwa kila kitu lakini tupo kwenye laana kubwa kwa kuongozwa na watunwenye akili ndogo, wanafiki, waongo na wqnaotegemea nguvu badala ya akili. Na hawawezi kutegemea akili kwa sababu hawana.
 

Malengo yako ni batili, maana badala ya kujikita na kujielekeza kuyapiku malengo yako, wewe unawaza kuwapiku watu ambao bado wako kwenye UMASIKINI.
Sasa wewe unaona watu hata chakula hawana, halafu wewe unataka kuwapiku.





 
Nani alikudanganya kuwa tumeachana na ujamaa? Chama kinachoongoza ni cha kijamaa na katiba inasema sisi ni wajamaa. Angalia mfano huu kuonyesha kuwa sisi bado ni wajamaa kindakindaki.

Leo imetangazwa kuwa mahindi huko Rukwa ni Tsh 20,000 kwa kilo mia. Kama mia mbili kwa kilo. Kwanini ipo hivyo? Ni kwa sababu serikali imebana watu kuuza mazao nje ya nchi. Inaweka zuio la moja kwa moja au inaweka vikwazo na tozo kibao. Watu hadi mahindi ya mwaka juzi wanayo. Kwenye nchi ambayo siyo ya kijamaa huwezi kupora nguvu ya mtu namna hiyo.
Hili suala matokeo yake ni kuwa wakulima wakubwa wa kibiashara hawalimi, wakulima wadogo wanakuwa maskini wakutupwa. Kilimo cha zana duni nk. Mfano serikali ingeachana na kilimo cha ujamaa naamini ndani ya 5 years tunaipita Kenya.

Baada ya Mao kufa China waliona ubaya wa kilimo cha ujamaa. Walichofanya, wakawaambia wakulima. Percent fulani ya mazao yako yatanunuliwa na serikali. Kinachobaki utauza kokote na kukifanyia vyovyote utakavyo. Mfano labda serikali inanunua 10 percent. 90 percent unauza utakako. Matokea yake kilimo kikakuwa maradufu ndani ya muda mfupi, na umaskini vijijini ukapungua kwa asilimia kubwa sana.

Usidanganyike. Ujamaa wetu hauwezi kuondoka wenyewe. Upo kwenye sheria zetu na taratibu za kuendesha nchi. Mpaka tutapoondoa ujamaa kwenye sheria na taratibu zetu ndipo utakapoondoka.
 
Miaka ya 80 Tanzania ilikiwa nchi yenye uchumi wa juu zaidi E.A ila A.Mwinyi alikuja kuua na kuturudisha nyuma
 
Fanya utafiti kabla ya kuzungumza
takwimu hazionyeshi kuwa tulikuwa na uchumi mkubwa kuliko Kenya. kwanza kwa utafiti mdogo miaka hiyo tulitoka kwenye vita ya Kagera, na Jumuia ya EA ilikuwa imevunjika , tukisubiri kugawana mali huku nyingi zikiwa Kenya. we utafiti gani umefanya unaoonyesha tulikuwa na uchui mkubwa?
 
Speed hatari ya kuelekea wapi?
 
Katibu mpya itakayotoa uhuru mkubwa na haki imara za kisiasa na kiuchumi.
 

ili tupige hatua hio ni lazima elimu na wananchi wajue kitu kinaitwa self reliance pamoja na wananchi kujion kama wanachama wa soko la dunia nzima, lazima tufanye kazi kwa bidii ukitanguliza ubunifu maana ndo unaouza sokoni, hilo ndo kubwa na option kubwa! mengine ni madogo madogo mfano siasa zikae vizuri , kila mtu atimize wajibu wake
 
Longterm:
1. Tuachane na elimu ya mkoloni na badala yake tuwe na elimu ya Mtanzania ya Kiswahili kwa masomo yote isipokuwa lugha za kigeni na kwa ngazi zote za elimu.

2. Katiba mpya.

Short term:
Hapa serikali inafanya vizuri kwa asilimia kubwa, usalama na mshikamano uko juu, rushwa iko chini na shughuli za maendeleo zinatekelezwa.

Muhimu wapunguze kuminya uhuru wa kisiasa na nafasi za uongozi ziwe merit based kuliko ilivyo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…