Serikali ifanye nini ili uchumi wetu uipiku Kenya na mataifa yenye uchumi mkubwa kuliko sisi?

Serikali ifanye nini ili uchumi wetu uipiku Kenya na mataifa yenye uchumi mkubwa kuliko sisi?

Kufuatana na tafiti za kitaalam, CCM imejaa watu wajinga. Unategemea mjinga akuongoze kuelekea kwenye maendeleo?

Chini ya uongozi wa CCM, hayo unayoyafikiria sahau. Tutaendelea kuwa mikia.
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Upo sahihi sana mkuu,hili swali lako ni paper kabisa linatakiwa lifanyiwe utafiti kabisa na wataalam ili waje na ufumbuzi wake mantashallah
 
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi na fulsa nyingi kwa nchi za afrika Mashariki.Tuna eneo kubwa la ardhi inayoweza kutumika kwa kilimo na ufugaji,tuna bahari, maziwa na Mito yenye samaki wa aina mbalimbali,tunayo madini ya aina mbalimbali nk.Karibu asilimia 60 ya wananchi wanajishughulisha na kilimo Cha kujikumu (njaa) na siyo kilimo biashara.wakulima wetu wanapambana Sana kutaka kufanya kilimo Cha kisasa na chenye Tija lakini wanakwamishwa na nyenzo za kufanyia kazi,(tractor au power tiler),pembejeo,miundo mbinu ya kusafirishia mazao kutoka mashambani na kufikisha sokoni bidhaa /mazao Yao au viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani nk.Hali ilivyo ni kwamba vijiji bado hawana wataalamu wa kilimo au mifugo na wakulima bado wanatumia majembe ya mikono ,mbolea au viatifu havipatikani kwa wakati/ havitoshelezi mahitaji ya wakulima.Bado kilimo chetu kinategemea mvua badala ya kuanza scheme za umwagiliaji,kilimo Cha kutegemea jembe la mkono na mvua,inakuwa vigumu kukopesheka na mabenki kutokana na uncertainty.Nini kifanyike: serikali iongeze bajeti ya kilimo kwa maana kilimo ni UTI wa mgongo na kinatoa ajira nyingi kwa watanzania Kama Kuna uwezekano kila Kijiji wapatiwe tractor ambalo litakodishwa kwa wahitaji kwa gharama nafuu( kwa ajili ya gharama za uendeshaji,) serikali kupitia Tarura wafanye matengenezo/maboresho ya barabara za vijijini ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima wakati wa kupeleka sokoni au viwanda vya kuchakata mazao,wizara ya viwanda na biashara kwa kushirikiana na wizara ya uwekezaji wahamasishe wawekezaji kujenga viwanda vidogo vidogo vya kimkakati katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kutafuta masoko vya mazao,vyama vya ushirika vilishiriki katika mchakato wa kuongeza thamani mazao na kutafuta masoko.Kuhusu upande wa bahari na maziwa,serikali ihamasishe wavuvi kutumia vyombo vya kisasa /Meli kufanya uvuvi na kuwa na vyombo vya kuhifadhia samaki.Benki ya kilimo na tib ziwe zinakwenda mikoani/wilayani kuangalia fulsa na kuwashawishi au kutoa elimu kwa vikindu mbalimbali juu ya huduma wanazotoa na faida zake kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu
Rasilimali zote hazina maana kama usipokuwa na uongozi wenye uwezo. Kwa sasa, nakadiria zaidi ya 80% viongozi wote, wana akili chini ya kiwango cha akili ya kawaida.

Tumebarikiwa kwa kila kitu lakini tupo kwenye laana kubwa kwa kuongozwa na watunwenye akili ndogo, wanafiki, waongo na wqnaotegemea nguvu badala ya akili. Na hawawezi kutegemea akili kwa sababu hawana.
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.

Malengo yako ni batili, maana badala ya kujikita na kujielekeza kuyapiku malengo yako, wewe unawaza kuwapiku watu ambao bado wako kwenye UMASIKINI.
Sasa wewe unaona watu hata chakula hawana, halafu wewe unataka kuwapiku.

IMG_2414.jpg


IMG_2414.jpg


IMG_2414.jpg
 
Nani alikudanganya kuwa tumeachana na ujamaa? Chama kinachoongoza ni cha kijamaa na katiba inasema sisi ni wajamaa. Angalia mfano huu kuonyesha kuwa sisi bado ni wajamaa kindakindaki.

Leo imetangazwa kuwa mahindi huko Rukwa ni Tsh 20,000 kwa kilo mia. Kama mia mbili kwa kilo. Kwanini ipo hivyo? Ni kwa sababu serikali imebana watu kuuza mazao nje ya nchi. Inaweka zuio la moja kwa moja au inaweka vikwazo na tozo kibao. Watu hadi mahindi ya mwaka juzi wanayo. Kwenye nchi ambayo siyo ya kijamaa huwezi kupora nguvu ya mtu namna hiyo.
Hili suala matokeo yake ni kuwa wakulima wakubwa wa kibiashara hawalimi, wakulima wadogo wanakuwa maskini wakutupwa. Kilimo cha zana duni nk. Mfano serikali ingeachana na kilimo cha ujamaa naamini ndani ya 5 years tunaipita Kenya.

Baada ya Mao kufa China waliona ubaya wa kilimo cha ujamaa. Walichofanya, wakawaambia wakulima. Percent fulani ya mazao yako yatanunuliwa na serikali. Kinachobaki utauza kokote na kukifanyia vyovyote utakavyo. Mfano labda serikali inanunua 10 percent. 90 percent unauza utakako. Matokea yake kilimo kikakuwa maradufu ndani ya muda mfupi, na umaskini vijijini ukapungua kwa asilimia kubwa sana.

Usidanganyike. Ujamaa wetu hauwezi kuondoka wenyewe. Upo kwenye sheria zetu na taratibu za kuendesha nchi. Mpaka tutapoondoa ujamaa kwenye sheria na taratibu zetu ndipo utakapoondoka.
 
Miaka ya 80 Tanzania ilikiwa nchi yenye uchumi wa juu zaidi E.A ila A.Mwinyi alikuja kuua na kuturudisha nyuma
 
Fanya utafiti kabla ya kuzungumza
takwimu hazionyeshi kuwa tulikuwa na uchumi mkubwa kuliko Kenya. kwanza kwa utafiti mdogo miaka hiyo tulitoka kwenye vita ya Kagera, na Jumuia ya EA ilikuwa imevunjika , tukisubiri kugawana mali huku nyingi zikiwa Kenya. we utafiti gani umefanya unaoonyesha tulikuwa na uchui mkubwa?
 
CCM under MagufuliJP tulikuwa na speed ya hatari. Hata wao waliona kabisa speed yetu wakaanza chuki. Ila kwasasa na speed ya mama. Tusahau kabisa tutanyonywa. Mshindani wako unatakiwa kuweka urafiki wenu kwa akili ila sisi tumekwemda mazima. Tutapigwa hatari sana
Speed hatari ya kuelekea wapi?
 
Katibu mpya itakayotoa uhuru mkubwa na haki imara za kisiasa na kiuchumi.
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.

ili tupige hatua hio ni lazima elimu na wananchi wajue kitu kinaitwa self reliance pamoja na wananchi kujion kama wanachama wa soko la dunia nzima, lazima tufanye kazi kwa bidii ukitanguliza ubunifu maana ndo unaouza sokoni, hilo ndo kubwa na option kubwa! mengine ni madogo madogo mfano siasa zikae vizuri , kila mtu atimize wajibu wake
 
Longterm:
1. Tuachane na elimu ya mkoloni na badala yake tuwe na elimu ya Mtanzania ya Kiswahili kwa masomo yote isipokuwa lugha za kigeni na kwa ngazi zote za elimu.

2. Katiba mpya.

Short term:
Hapa serikali inafanya vizuri kwa asilimia kubwa, usalama na mshikamano uko juu, rushwa iko chini na shughuli za maendeleo zinatekelezwa.

Muhimu wapunguze kuminya uhuru wa kisiasa na nafasi za uongozi ziwe merit based kuliko ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom