Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo sahihi sana mkuu,hili swali lako ni paper kabisa linatakiwa lifanyiwe utafiti kabisa na wataalam ili waje na ufumbuzi wake mantashallahKama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.
Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Rasilimali zote hazina maana kama usipokuwa na uongozi wenye uwezo. Kwa sasa, nakadiria zaidi ya 80% viongozi wote, wana akili chini ya kiwango cha akili ya kawaida.Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi na fulsa nyingi kwa nchi za afrika Mashariki.Tuna eneo kubwa la ardhi inayoweza kutumika kwa kilimo na ufugaji,tuna bahari, maziwa na Mito yenye samaki wa aina mbalimbali,tunayo madini ya aina mbalimbali nk.Karibu asilimia 60 ya wananchi wanajishughulisha na kilimo Cha kujikumu (njaa) na siyo kilimo biashara.wakulima wetu wanapambana Sana kutaka kufanya kilimo Cha kisasa na chenye Tija lakini wanakwamishwa na nyenzo za kufanyia kazi,(tractor au power tiler),pembejeo,miundo mbinu ya kusafirishia mazao kutoka mashambani na kufikisha sokoni bidhaa /mazao Yao au viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani nk.Hali ilivyo ni kwamba vijiji bado hawana wataalamu wa kilimo au mifugo na wakulima bado wanatumia majembe ya mikono ,mbolea au viatifu havipatikani kwa wakati/ havitoshelezi mahitaji ya wakulima.Bado kilimo chetu kinategemea mvua badala ya kuanza scheme za umwagiliaji,kilimo Cha kutegemea jembe la mkono na mvua,inakuwa vigumu kukopesheka na mabenki kutokana na uncertainty.Nini kifanyike: serikali iongeze bajeti ya kilimo kwa maana kilimo ni UTI wa mgongo na kinatoa ajira nyingi kwa watanzania Kama Kuna uwezekano kila Kijiji wapatiwe tractor ambalo litakodishwa kwa wahitaji kwa gharama nafuu( kwa ajili ya gharama za uendeshaji,) serikali kupitia Tarura wafanye matengenezo/maboresho ya barabara za vijijini ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima wakati wa kupeleka sokoni au viwanda vya kuchakata mazao,wizara ya viwanda na biashara kwa kushirikiana na wizara ya uwekezaji wahamasishe wawekezaji kujenga viwanda vidogo vidogo vya kimkakati katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kutafuta masoko vya mazao,vyama vya ushirika vilishiriki katika mchakato wa kuongeza thamani mazao na kutafuta masoko.Kuhusu upande wa bahari na maziwa,serikali ihamasishe wavuvi kutumia vyombo vya kisasa /Meli kufanya uvuvi na kuwa na vyombo vya kuhifadhia samaki.Benki ya kilimo na tib ziwe zinakwenda mikoani/wilayani kuangalia fulsa na kuwashawishi au kutoa elimu kwa vikindu mbalimbali juu ya huduma wanazotoa na faida zake kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.
Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Uchumi mkubwa! Uongo utakuwa ulienezwa na mwenyekiti.Miaka ya 80 Tanzania ilikiwa nchi yenye uchumi wa juu zaidi E.A ila A.Mwinyi alikuja kuua na kuturudisha nyuma
Fanya utafiti kabla ya kuzungumzaUchumi mkubwa! Uongo utakuwa ulienezwa na mwenyekiti.
takwimu hazionyeshi kuwa tulikuwa na uchumi mkubwa kuliko Kenya. kwanza kwa utafiti mdogo miaka hiyo tulitoka kwenye vita ya Kagera, na Jumuia ya EA ilikuwa imevunjika , tukisubiri kugawana mali huku nyingi zikiwa Kenya. we utafiti gani umefanya unaoonyesha tulikuwa na uchui mkubwa?Fanya utafiti kabla ya kuzungumza
Speed hatari ya kuelekea wapi?CCM under MagufuliJP tulikuwa na speed ya hatari. Hata wao waliona kabisa speed yetu wakaanza chuki. Ila kwasasa na speed ya mama. Tusahau kabisa tutanyonywa. Mshindani wako unatakiwa kuweka urafiki wenu kwa akili ila sisi tumekwemda mazima. Tutapigwa hatari sana
Uliza vitu vya maana, Kama vile kuipiku Malaysia siyo Kenya masikini wenzetu.
Kupunguza au kuongeza kodi ni kazi ya bungeSerikali ipunguze kodi tu . Baasu
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.
Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.