Serikali ifikirie kupunguza muda wa kusoma darasani, vijana wanazeekea shuleni!

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Ukweli ni kwamba mambo mengi yanayofundishwa shule ya msingi ndio hayo hayo yanafunzwa shule ya sekondari. Ushauri wangu ifanyike review ya mitaala ya elimu yetu na masomo yanayowezesha elimu ya kujitegemea yaongezwe.

Tupunguze mfumo wa elimu ya white colar na badala yake tuweke mfumo wa elimu unaojenga watu kujitegemea zaidi. Muda wa kukaa shuleni upunguzwe ikiwezekana chini ya miaka 23 ya umri wa kuishi kijana anaetakiwa kuajiriwa aajiriwe na anaetakiwa kwenda kujiajiri aende kujiajiri.

Kama masomo ya KILIMO, BIASHARA na UJASIRIAMALI hayataongezwa kwenye mitaala yetu kujiajiri kwenye tija itakuwa shida.

Nawasilisha.
 
Hoja nzuri Ila kumbuka hatupangiwi,acha hivyo hivyo tuendelee na mfumo kikoloni wasije zinduka akili haujui tuna mpango chama chetu kitawale milele? (Alisikika kada mtiifu)
 
Naunga mkono hoja
Watu wanatumia karibia robo ya umri wa kuishi shuleni hiyo inakatisha tamaa wazazi na hao watafuta elimu....wastani mtu mpaka aanze kujitegemea baada ya shule ni miaka 28 hivi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…