Serikali ifikirie kwa kina kuwa na "Shirika la Maji la Taifa" na pia kuanzisha "Rural Water Access Agency" ya maji vijijini kama umeme wa REA

Serikali ifikirie kwa kina kuwa na "Shirika la Maji la Taifa" na pia kuanzisha "Rural Water Access Agency" ya maji vijijini kama umeme wa REA

Hapana Mkuu. Ni kwamba siku hizi suala la maji liko kwa kiasi fulani liko halmashauri za miji, lakini kumbuka halmashauri za miji haziko chini ya wizara ya maji, ziko chini ya Tamisemi na bado maji ni jukumu la Waizara ya maji. Ndio maana nikasema hii inaleta mkanganyiko tu. Suala ni kuondoa maji halmashauri za miji na Wizara ya maji na kuanzisha shirika linalojitegemea chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kama mashirika mengine ya umma.
Hazi mamlaka zipo chini ya halmashauri au wizara ya maji. Mfano dawasa na dawasco zipo chini ya nani?
 
Hazi mamlaka zipo chini ya halmashauri au wizara ya maji. Mfano dawasa na dawasco zipo chini ya nani?
Kwa kiwango kikubwa zinaendeshwa chini ya serikali za miji. Hivyo utakuta maamuzi mengi yanakuwa ya madiwani nk. Ndipo lilipokuja wazo la kuwa na bodi za maji, ambazo zinawajibika kwa wizara ya maji. Makumbuka Kitila Mkumbo amekuwa mhamasishaji wa bodi hizi.

Lakini sasa, utakuta miradi ya maji inakuwa chini ya mhandisi wa maji wa wilaya au mkoa, ambaye ni mwajiriwa wa serikali chini ya wizara ya maji.

Ndio maana nikasema yaani mambo yamekorogwa vitu havieleweki kabisa.
 
Watu wanasema unapokuwa na njia ambayo kwa miaka mingi haizai matunda na bado unaing'ang'ania badala ya kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo, wewe una tatizo la akili.

Suala la upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi, mijini na vijijini, limekuwa jambo ambalo limeumiza kichwa serikali kwa miaka mingi sana. Kuna wakati huduma hii ilikuwa chini ya mamlaka ya serikali mija kwa moja - Idara ya Maji chini wa Wizara. Hili halikufaniliwa.

Utaratibu wa huduma za maji uliopo sasa ndio unachanganya kuliko hata huko nyumba. Tunashindwa kuelewa nani hasa ndio mwenye mamlaka kaitika suala la maji. Unakuta Wiara ipo, na serikali za miji zipo, na mwisho wa siku haieleweki nani ana mamlaka zaidi ya mwenzake.

Kuna Board za maji zimeanzishwa lakini ni kama hazina meno, zipo zipo tu!

Sasa wakati umefika tutafute namna mpya ya kushughulika na suala la maji nchini. Tunapaswa kufikira kwa makini uwepo wa Shirika la Maji la Taifa, ambalo majukumu yake yatakuwa kama lilivyo TANESCO, na pia kuwa na Rural Water Access Agency, ambayo majukumu yake yatakuwa kama ilivyo REA. Shirika hili linaweza kuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kulipa uzito au Wizara ya Maji ikibidi

Kwa upande wa Shrika la Maji, hili litapaswa kujiendesha kibiashara. kwa ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya. Ruzuku toka serikalini inaweza kuwapo mwanzoni lakini baada ya muda fulani tutatarajie lijiendeshe kwa faida.

Ni kweli huko nyuma tulikuwa na NUWA (National Urban Water Authority) , na lengo lilikuwa zuri bali lilikumbwa na mihemuko ya kisiasa enzi za ubinafsishaji likatenguliwa. Tuanzishe kitu bora zaidi.

Rural Water Access Agency, kama ilivyo REA, itapewa ruzuku toka serikalini, na pia kutakuwa na levy (tozo) toka kwenye bili za maji za Shirika la Maji la Taifa kwa ajili ya kuendeleza upatikanaji wa maji vijijini.

Ningependa sana Kitila Mkumbo watafakari kwa makini pendekezo hili na kulifikisha kwa Magufuli ili lifanyiwe utekelezaji.
Ndugu yangu unamawazo mazuri sana lakini inawezekana wewe sio mfuatiliaji mzuri wa mambo yanavyokwenda. Serikali kupitia Wizara ya Maji imeanzisha Wakala mpya inayoitwa Wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira Vijijini kwa kifupi RUWASA hii ilienda sanjari na kufuta iliyokuwa wakala wa uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa ambayo imeiunganishwa na hii Wakala Mpya.RUWASA ilianza kazi rasmi mwaka jana tarehe 1/7/2019 baada ya sheria ya uanzishwaji wake kupitishwa na Bunge. Idara za maji zote kwenye Halmashauri zimehamishiwa RUWASA, Hii Wakala jukumu lake kubwa ni kuhakikisha Vijiji vyote nchini vinapata maji safi na salama.Ina ofisi kila wilaya na kila mkoa kasoro Dar es salaam.Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti ya wizara ya Maji (www.maji.go.tz)
 
Mh with due respect, ulichokisema ni kweli kabisa! Kwa sasa Tanzania Bara tuna aina mbili za utoaji wa huduma ya maji nchini kwanza pale Wizarani kuna idara ya Maji Mijini ambayo chini yake kuna hizi Mamlaka za Maji za Miji Mikuu,Miji Midogo na Makao makuu ya Wilaya (Huitwa Water Authoritoes kawa DAWASA,MWAUWASA n.k).

Kwa upande wa maji Vijijini kuna Agency (Wakala wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira/maji taka Vijijini) mahsusi imeanzishwa chini ya sheria Namba 5 ya mwaka 2019(Fuatilia uanzishwaji wake na majukumu yake) hii inaitwa RUWASA (Rural Water Supply and Saniatation Agency),Hii Taasisi/Wakala haina muda mrefu ndiyo maana huajaisiskia sana. Changamoto iliyopo kubwa ni wao kujitangaza na Serikali kuhakikisha hii Taasisi inawezeshwa vizuri ili iweze kufanya kazi zake kikamilifu. (Suala la Source of income kwa Taasisi ndiyo la kuzingatiwa zaidi maana tunaweza kuwa na Taasisi kibao lakini bila chanzo cha mapato cha uhakika hakitafanyika chochote)
 
Ndugu yangu unamawazo mazuri sana lakini inawezekana wewe sio mfuatiliaji mzuri wa mambo yanavyokwenda. Serikali kupitia Wizara ya Maji imeanzisha Wakala mpya inayoitwa Wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira Vijijini kwa kifupi RUWASA hii ilienda sanjari na kufuta iliyokuwa wakala wa uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa ambayo imeiunganishwa na hii Wakala Mpya.RUWASA ilianza kazi rasmi mwaka jana tarehe 1/7/2019 baada ya sheria ya uanzishwaji wake kupitishwa na Bunge. Idara za maji zote kwenye Halmashauri zimehamishiwa RUWASA, Hii Wakala jukumu lake kubwa ni kuhakikisha Vijiji vyote nchini vinapata maji safi na salama.Ina ofisi kila wilaya na kila mkoa kasoro Dar es salaam.Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti ya wizara ya Maji (www.maji.go.tz)
NI jambo jema kama hilo limefanyika.

Hata hivyo bado kuna kasoro. Ninachoona ni kwamba RUWASA inaendeshwa na serikali kupitia Wizara ya Maji. Labda ni kwa kuwa RUWASA wanaona hawawezi kujiendesha kibiashara kwa kuwa huduma ya maji vijijini ni suala la social service zaidi ya commercial service.

Bado ningependa RUWASA iwe na mfumo kama wa REA, ambapo inakuwa ina autonomy ambayo inaiondoa kiasi fulani kusimamiwa moja kwa moja na serikali katika utendaji wa kila siku. Historia imeshatuonyesha vitu vinavyosimamiwa moja kwa moja na wizara mara nyingi havifanikiwi, na ndio lengo la kubadilisha idara nyingi za serikali na kuzifanya Agency. Mifano ni mingi, Meteorology na Wizara ya Mawasiliano; TPDC na Wizara ya Nishati; REA na Wizara ya Nishati , TCCL na wizara ya mawasiliano etc
 
Halafu Mkuu kuna kitu nimekiona kwenye hiyo website ya maji kinatoa food for thought pia. Nimeona EWURA imeorodhoshwa kama taasisi ya Wizara ya Maji. Bila Shaka wizara ya Nishati pia itairodhesha EWURA kama taaisi yake. Sasa mwisho wa mambo yote, Mkurugenzi wa EWURA anawajibika kwa Waziri gani katika mambo ya policy zaidi ya Board ya EWURA yenye kutoa executive guidance?

Haya ndio mambo nasema yanachanganya kidogo. Je, hili lilifanywa kupunguza gharama za kuwa na Water Regulatory Authority inayojitegemea? Labda kama huduma ya maji imeegemea zaidi serikalini, basi hakuna haja ya kuwa na water regulatory authority
 
EWURA ni Taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya Maji na CEO wake anawajibika kwa KM wa wizara ya maji na sio Wizara ya Nishati kama unavyohisi.
 
Pamoja na hizo taasisi bado maji shida ..yaani unafuu ni tunapata kwa zamu Leo hayatoki au wiki
Nashikuru umeuniulizia swali langu
Au jamaa anahitaji ulaji?
Ukiwa mlaji au unatumia raslimali vibaya ..in short ukiwa mwizi basi kila mtu utadhani anaiba
 
EWURA ni Taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya Maji na CEO wake anawajibika kwa KM wa wizara ya maji na sio Wizara ya Nishati kama unavyohisi.
Sasa hapo mbona itakuwa ni mkanganyiko sana. Kumbuka kazi za EWURA ni hizi;

The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an autonomous multi-sectoral regulatory authority established by the EWURA-Act-Cap-414 of the laws of Tanzania. It is responsible for technical and economic regulation of the electricity, petroleum, natural gas and water sectors in Tanzania pursuant to Cap 414 and sector legislation.

EWURA hawawezi kufanya kazi zote hizo za nishati umeme, mafuta na gesi - kwa kusimamiwa na waziri wa maji. Na unapotaja sekta, Sheria iliyoanzisha EWURA inamtaja waziri kama ifuatavyo

1591799693908.png

Kwa jinsi hiyo basi, EWURA hawawezi kufanya maamuzi ya sekta ya nishati kwa mamlaka ya waziri wa maji, bali wa Nishati, na maamuzi mambo ya maji yatafanywa kwa mamlaka ya Waziri wa Maji.

Ndio nikasema, hii inafanya EWURA wasiwe na namna ya kuwajibishwa na waziri yeyote, na ingebidi Regulator wa maji atenganishwe na yule wa nishati ili kuwe na uwajibikaji unaoeleweka.

Na ukiweka Regulator wa maji basi atasimamia usambazaji maji, uagizaji maji toka nje, uzalishaji maji (pamoja na ya chupa), matumizi ya maji ya mito na maziwa (pamoja na kuzalisha umeme), na matumizi ya maji ya visima (uchimbaji visima), utengenezaji mabwawa ya maji
 
Back
Top Bottom