Serikali iingilie kati wizi unaofanywa na Halotel

John Gregory

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2019
Posts
1,137
Reaction score
2,147
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Halotel katika menu ya weekly mega bundle ambayo ulikuwa ukipatiwa dakika 30 mitandao yote dakika 30 halotel na mb 1000 waliamua kukipunguza mpaka kufikia mb 600 kwa wiki. Kama hiyo haitoshi jana jioni waliamua kudanganya watumiaji wake kwa kuandika kwamba kwa sasa kwa sh 1000 utapata mb 800 cha kushangaza baada ya kujiunga unatumiwa message kwamba umepata mb 500 badala ya 800 iliyoonekana hapo awali ikiwa ni pungufu ya mb 300.

Huu ni WIZI mkubwa!.Ni sawa na kwenda dukani ukaona bidhaa nje ya box wameandika ndani kuna pieces 12 kisha baada ya kununua ukakuta pieces 5!

Cha ajabu wao siku zote marekebisho yao yanawaathiri watumiaji tu na wanaishia kukuomba radhi lakini haijawahi kutokea yakawaathiri wao! Na hata ikitokea wapo tayari kurudishia gharama zao zilizopotea! Lakini kwa wewe mtumia utaombwa radhi TU!

HII SIO SAWA!

Kama kuna mawakili humu tuungane kuifungulia kesi HALOTEL kwa maana huu ni wizi wa wazi wazi na ushahidi wote upo!
 
Mkuu sio hao tu karibia mitandao yote hapa Tz yana shida' Jana niliweka salio la 1000 tigo na kujiunga naambiwa sina salio na kuwapigia eti kuna tatizo la kimtandao ila hela yangu ipo alaf kuwapigia tena mbona hamna salio yaan wanakukatia simu as if it's okay kabisa na wanachofanya' BONGO NYOSO FULLY BULLSHIT
 
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Halotel katika menu ya weekly mega bundle ambayo ulikuwa ukipatiwa dakika 30 mitandao yote dakika 30 halotel na mb 1000 waliamua kukipunguza mpaka kufikia mb 600 kwa wiki. Kama hiyo haitoshi jana jioni waliamua kudanganya watumiaji wake kwa kuandika kwamba kwa sasa kwa sh 1000 utapata mb 800 cha kushangaza baada ya kujiunga unatumiwa message kwamba umepata mb 500 badala ya 800 iliyoonekana hapo awali ikiwa ni pungufu ya mb 300.

Huu ni WIZI mkubwa!.Ni sawa na kwenda dukani ukaona bidhaa nje ya box wameandika ndani kuna pieces 12 kisha baada ya kununua ukakuta pieces 5!

Cha ajabu wao siku zote marekebisho yao yanawaathiri watumiaji tu na wanaishia kukuomba radhi lakini haijawahi kutokea yakawaathiri wao! Na hata ikitokea wapo tayari kurudishia gharama zao zilizopotea! Lakini kwa wewe mtumia utaombwa radhi TU!

HII SIO SAWA!

Kama kuna mawakili humu tuungane kuifungulia kesi HALOTEL kwa maana huu ni wizi wa wazi wazi na ushahidi wote upo!
Mi nilishawahama muda ,wapumbavy! Imebaki tu line hewani ila sijiungi na chochote km nilivyowanyia voda
 
Dah hakika sina cha kusema kuhusu huu mtandao

Dakika kumi nyuma nimetoka kuongea nao ila nawakubali ila madhaifu ni menGi hasa ya kitandao
 
Aloo halotel ni wasumbufu. Nimejaza umeme hela wamekata token hawanipi kila ukipiga simu wanakuambia tutatuma zaidi ya siku nne sasa
 
Sio sawa kujilinganisha na nchi zilizoendelea lakini nchi kama marekani watu hawanunui vifurushi vya kupimiwa au rejareja kama ngano.
Bali wametandaza fiber kila sehemu ni wewe tu kuvuta nyumbani kwako unalipia kwa mwezi unlimited kwa speed fulani.
Labda kama mtu yupo mbali na nyumbani kwake ndio atanunua vya mobile, kizuri hata mitaani kuna public wi-fi.

TTCL huu ndio wakati bora wa kufanya maamuzi kama haya na kuwa na ushindani mkubwa wa kibiashara ambao haujawahi kutokea tanzania.
Hii itawapiga chini mitandao yote inayofuja pesa za watanzania kwa Data za kupima.

Cha kufanya ni watandaze fiber karibu mitaa yote ya dar, kuhusu ugeni wa watu kwenye hili jambo ni kwamba wakizoea tu basi wataanza kutumia kama zilivyoanza smartphones.
Ndani ya miaka 3 au 5 wananchi watakuwa wameshazoea.

Kama vifurushi vitakuwa vya bei ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu mfano kifurushi cha chini kabisa kikianzia elfu 25,000 kwa mwezi basi lazima watu wengi wavutiwe.
Ni kama vifurushi vya ving'amuzi tu, bei ni kama hiyo lakini watu wananunua.

Hata kama gharama za utekelezaji wa mpango zitakuwa kubwa lakini in long term hili litakuwa na faida isiyo na kikomo.
Kumbuka kuwa wa kwanza ndio kila kitu, kama TTCL akianza basi atadominate na kushikilia soko lote.

TTCL lazima watakuwa wanapita humu hivyo mkiona hii post basi wananchi wanaomba mfanye hivyo.
Nadhani mpaka mwakani TTCL wanaweza kuwa tayari wameshakamilisha hili jambo.
 
Hata mimi nimewakataa kwa sababu ya wizi wa Mb yaani nikiangalia kwenye matumizi ya data nakuta nimetumia Mb 400 na point Ktk 600 halafu tayari wameshakata bando na kutuma sms kamba sina Salio la kutosha , nikabadilisha kifuruahi nikawa najiunga mega eflu 3 gb 2 hali bado ile ile hapo ndio nikaikacha rasmi

Nimeicha halotel kwa sababu ya kusapoti freebasic kunisaidia kuzama Jf wkt sina bando lasivyo kitambo ningeitupa chooni.
 
Kama mwanzo wa mwaka vifurushi vinauzwa bei hii, navuta picha kufika october sijui hali itakuwaje
 
Sio sawa kujilinganisha na nchi zilizoendelea lakini nchi kama marekani watu hawanunui vifurushi vya kupimiwa au rejareja kama ngano.
Bali wametandaza fiber kila sehemu ni wewe tu kuvuta nyumbani kwako unalipia kwa mwezi unlimited kwa speed fulani.
Labda kama mtu yupo mbali na nyumbani kwake ndio atanunua vya mobile, kizuri hata mitaani kuna public wi-fi.

TTCL huu ndio wakati bora wa kufanya maamuzi kama haya na kuwa na ushindani mkubwa wa kibiashara ambao haujawahi kutokea tanzania.
Hii itawapiga chini mitandao yote inayofuja pesa za watanzania kwa Data za kupima.

Cha kufanya ni watandaze fiber karibu mitaa yote ya dar, kuhusu ugeni wa watu kwenye hili jambo ni kwamba wakizoea tu basi wataanza kutumia kama zilivyoanza smartphones.
Ndani ya miaka 3 au 5 wananchi watakuwa wameshazoea.

Kama vifurushi vitakuwa vya bei ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu mfano kifurushi cha chini kabisa kikianzia elfu 25,000 kwa mwezi basi lazima watu wengi wavutiwe.
Ni kama vifurushi vya ving'amuzi tu, bei ni kama hiyo lakini watu wananunua.

Hata kama gharama za utekelezaji wa mpango zitakuwa kubwa lakini in long term hili litakuwa na faida isiyo na kikomo.
Kumbuka kuwa wa kwanza ndio kila kitu, kama TTCL akianza basi atadominate na kushikilia soko lote.

TTCL lazima watakuwa wanapita humu hivyo mkiona hii post basi wananchi wanaomba mfanye hivyo.
Nadhani mpaka mwakani TTCL wanaweza kuwa tayari wameshakamilisha hili jambo.
Hao fibre, ttcl wakishapata wateja nao watafanya fujo za kuongeza gharama kama ambavyo mitandao inafanya

Halotel walianza na MB600 za wiki kwa jero, ilikuwa ni ngumu kwa wakati huo ku picture kuja kuuziwa hiki kifurushi cha MB500 kwa bei hii
 
Back
Top Bottom