Serikali iingilie kati wizi unaofanywa na Halotel

Serikali iingilie kati wizi unaofanywa na Halotel

Sio sawa kujilinganisha na nchi zilizoendelea lakini nchi kama marekani watu hawanunui vifurushi vya kupimiwa au rejareja kama ngano.
Bali wametandaza fiber kila sehemu ni wewe tu kuvuta nyumbani kwako unalipia kwa mwezi unlimited kwa speed fulani.
Labda kama mtu yupo mbali na nyumbani kwake ndio atanunua vya mobile, kizuri hata mitaani kuna public wi-fi.

TTCL huu ndio wakati bora wa kufanya maamuzi kama haya na kuwa na ushindani mkubwa wa kibiashara ambao haujawahi kutokea tanzania.
Hii itawapiga chini mitandao yote inayofuja pesa za watanzania kwa Data za kupima.

Cha kufanya ni watandaze fiber karibu mitaa yote ya dar, kuhusu ugeni wa watu kwenye hili jambo ni kwamba wakizoea tu basi wataanza kutumia kama zilivyoanza smartphones.
Ndani ya miaka 3 au 5 wananchi watakuwa wameshazoea.

Kama vifurushi vitakuwa vya bei ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu mfano kifurushi cha chini kabisa kikianzia elfu 25,000 kwa mwezi basi lazima watu wengi wavutiwe.
Ni kama vifurushi vya ving'amuzi tu, bei ni kama hiyo lakini watu wananunua.

Hata kama gharama za utekelezaji wa mpango zitakuwa kubwa lakini in long term hili litakuwa na faida isiyo na kikomo.
Kumbuka kuwa wa kwanza ndio kila kitu, kama TTCL akianza basi atadominate na kushikilia soko lote.

TTCL lazima watakuwa wanapita humu hivyo mkiona hii post basi wananchi wanaomba mfanye hivyo.
Nadhani mpaka mwakani TTCL wanaweza kuwa tayari wameshakamilisha hili jambo.
Mkuu umeandika vizuri sana na inaonekana wewe ni mtaalamu wa haya mambo.

Lakini kwa hoja yako mimi ninabishi kuwezekana Tz kwa kupitia Ttcl kupitia utawala huu.

Ttcl ndiyo "baba" la mawasiliano nchini na ndiyo shirika la Taifa la mawasiliano.

Cha kujiuliza: kwanini washindwe kuunganisha Taifa ki mtandao wa mawasiliano na kwa nini washindwe kupunguza gharama za bando na matumizi yote ya simu?

Kumbe sasa usilolijua ndiyo linakupa matumaini kwamba Ttcl wanaweza kufanya kwa mafanikio yote uyawazayo, jambo hilo haliwezekani.

Hivi kwa serikali hii ya awamu ya 6 jinsi wanavyochukuliana waweza kuamini shirika la umma linaweza kuondoa ama kupunguza kero za raia Tz?

Kuna mumiani wavurugaji ambao kazi yao ni kuzuia kupunguza ama kushawishi kuhusu kupandisha bei, wamekaa kama mashetani hawana rangi wala sura, lakini wapo.

Jambo hilo ni gumu sana.
 
Karibu Airtel wezi wengine
Ukinunua mb500 ukifungua Instagram ukasoma post mbili za Mwijaku unaambiwa umeshatumia 75%
 
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Halotel katika menu ya weekly mega bundle ambayo ulikuwa ukipatiwa dakika 30 mitandao yote dakika 30 halotel na mb 1000 waliamua kukipunguza mpaka kufikia mb 600 kwa wiki. Kama hiyo haitoshi jana jioni waliamua kudanganya watumiaji wake kwa kuandika kwamba kwa sasa kwa sh 1000 utapata mb 800 cha kushangaza baada ya kujiunga unatumiwa message kwamba umepata mb 500 badala ya 800 iliyoonekana hapo awali ikiwa ni pungufu ya mb 300.

Huu ni WIZI mkubwa!.Ni sawa na kwenda dukani ukaona bidhaa nje ya box wameandika ndani kuna pieces 12 kisha baada ya kununua ukakuta pieces 5!

Cha ajabu wao siku zote marekebisho yao yanawaathiri watumiaji tu na wanaishia kukuomba radhi lakini haijawahi kutokea yakawaathiri wao! Na hata ikitokea wapo tayari kurudishia gharama zao zilizopotea! Lakini kwa wewe mtumia utaombwa radhi TU!

HII SIO SAWA!

Kama kuna mawakili humu tuungane kuifungulia kesi HALOTEL kwa maana huu ni wizi wa wazi wazi na ushahidi wote upo!
Usihofu Nape atashughulikia hili
 
Hata mimi nimewakataa kwa sababu ya wizi wa Mb yaani nikiangalia kwenye matumizi ya data nakuta nimetumia Mb 400 na point Ktk 600 halafu tayari wameshakata bando na kutuma sms kamba sina Salio la kutosha , nikabadilisha kifuruahi nikawa najiunga mega eflu 3 gb 2 hali bado ile ile hapo ndio nikaikacha rasmi

Nimeicha halotel kwa sababu ya kusapoti freebasic kunisaidia kuzama Jf wkt sina bando lasivyo kitambo ningeitupa chooni.
Mkuu unaipataje hiyo free basic ya kuingia Jf bila bando? Maana mim nimeitafuta bila mafanikio
 
Mkuu unaipataje hiyo free basic ya kuingia Jf bila bando? Maana mim nimeitafuta bila mafanikio
unabofya www. Freebasics. com kwenye browser haswa chrome hapo unapeta tu lkn app yake inazingua.Kisha utakutana na wikipedia ,bbc Swahili nk km Jf haipo nenda kwny kuongeza huduma za kutumia utaikuta then una iadd mchezo unaisha mda wowote online.
 
Karibu Airtel wezi wengine
Ukinunua mb500 ukifungua Instagram ukasoma post mbili za Mwijaku unaambiwa umeshatumia 75%
Hahaha!! mm siwasahau Airtel mb 600 ziliisha kwa notifications za wasap na You2be mpk leo nimejiwekea sitotumia mimi na wao maadili forever .
 
unabofya www. Freebasics. com kwenye browser haswa chrome hapo unapeta tu lkn app yake inazingua.Kisha utakutana na wikipedia ,bbc Swahili nk km Jf haipo nenda kwny kuongeza huduma za kutumia utaikuta then una iadd mchezo unaisha mda wowote online.
Shukran mkuu
 
Kila cku Hawa jamaa wanapunguza tuh mim ninamwez huu neona bora nihie tigo kdogo napata unafuu, Ila Hawa jamaa ni hatar,,,
 
Mm saizi nimeamua Bora nitoe 1500 nipate GB 1 Tigo ,kuliko hao wajinga hallotel 1000 MB 600 na hizo MB zenyewe kama MB 100 tu . Mwezi wa pili huu sijaunga bando Wala sms hallotel
 
halotel ni wahuni waliojificha kwenye biashara ya mtandao wa simu.nilikosea kutuma pesa kwenye namba ya tigo. Baada ya kuwapigia wakasema pesa imeshaenda tigo. nikawapigia tigo wakablock pesa kisha wakairudisha halotel

Halote walikubali pesa imeingia kwao nisubiri ndani ya saa 48 nitapokea.kila nikipiga simu ahadi haziishi. nikaenda ofisini kwao wanipanga njoo tarehe fulani mpaka nikachoka kuifuatilia.

suala la vocha ukiweka ukiambiwa haipo ni kawaida. ukipiga simu mchana wanapokea kesho yake asubuhi nà sound juu
 
Back
Top Bottom