Serikali ijenge barabara za kulipia Dar es salaam ili watu wafike kazini mapema

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Dar es salaam ina kanda kuu kama nne hivi, KANDA YA GONGOLAMBOTO na viunga vyake, KANDA YA MBAGARA na viunga vyake, KANDA YA MBEZI BEACH na viunga vyake na KANDA YA MBEZI LOUIS/KIMARA na viunga vyake.

Serikali ijenge barabara katika kanda hizi.

Barabara ziwe za kulipia angalau 2000-5000 kwa gari binafsi na 5000-10000 kwa gari za abiria.

Hizi barabara ziwe na vituo vichache tu na speed ni kuanzia 80 km/h - 120 km/h. Chini ya speed hiyo ni faini.

Hapo mtu utaweza kuondoka Tegeta saa moja na nusu na kufika kazini Posta saa mbili kamili
 
Tena ziwe barabara za juu mtu ukiondoka posta kituo mwenge then tegeta
 
Mtoa hoja kumbuka sisi bado ni wajamaa, hatujawahi kuukana ujamaa wetu popote pale.
Mulamula anasema sisi tuko neutral.

Lakini ni nchi gani ya Ujamaa inalipa mshahara kwa watumishi kwa utofauti kiasi hichi cha Tanzania?

Mmoja analipwa 300,000 anaambiwa ajitegemee chakula, malazi, mavazi n.k

Huku mwingine analipwa 15,000,000 huku akipewa mahitaji mengine bure.
 
Mleta mada naona umeshakubali hii serikali ya CCM ni chakavu viongozi wake hawana tena mbinu mpya za kuleta maendeleo, hivyo umeona jambo la msingi ni kurudi kumkamua mtanzania yule yule anayelipa kodi kila wakati ila umuhimu wa hiyo kodi yake hauonekani.

Naona kama taifa tulikimbilia kupata uhuru bila kujua nini tutafanya baada ya kupata uhuru huo, tunazidi kurudi nyuma kila siku kimaendeleo kwa fikra zetu zakitumwa.
 
Pesa zipo nyingi, wachukue hizo pesa wajenge hizo barabara
 
Siungi mkono hoja. Badala yake naishauri serikali iendelee kubuni mbinu mbadala za kupunguza foleni. Na moja wapo ni kuimarisha/kuboresha miundombinu ya usafiri wa umma, ili kupunguza matumizi ya usafiri binafsi.

Yaani ikiwezekana zijengwe njia za reli ya kisasa kabisa ya mwendokasi Jiji zima kama ilivyo huko kwa wenzetu, ili kumuwesesha mtu kufika sehemu kwa wakati. Vipanya na coaster zifutiliwe mbali. Badala yake yaruhusiwe mabasi makubwa pekee kubeba abiria.

Pia zingetengenezwa service road za kutosha kwa ajili ya waenda kwa miguu, waendesha baiskeli na bodaboda!

Na mwisho wa siku watu wa Dar mpunguze uvivu! Yaani hata umbali wa mita 2 tu, mtu anapanda daladala! Mnashindwa kuniiga mimi wakati nasoma hapo Udsm!

Nilikuwa kila siku nakanyaga kwa miguu kutoka Mabibo Hostel nilikokuwa nimebebana na jamaa, mpaka Main Campus! Na bado nilikuwa nawahi kipindi cha saa 1 asubuhi pale Nkrumah Hall.
 
Mleta mada naona umeshakubali hii serikali ya CCM ni chakavu viongozi wake hawana tena mbinu mpya za kuleta maendeleo, hivyo umeona jambo la msingi ni kurudi kumkamua mtanzania yule yule anayelipa kodi kila wakati ila umuhimu wa hiyo kodi yake hauonekani.

Naona kama taifa tulikimbilia kupata uhuru bila kujua nini tutafanya baada ya kupata uhuru huo, tunazidi kurudi nyuma kila siku kimaendeleo kwa fikra zetu zakitumwa.
Jiwe ndiye chanzo cha yote haya mkuu, kifupi ccm walikosea sana kumpa nchi.
 
Mulamula anasema sisi tuko neutral.
Lakini ni nchi gani ya Ujamaa inalipa mshahara kwa watumishi kwa utofauti kiasi hichi cha Tanzania?
Mmoja analipwa 300,000 anaambiwa ajitegemee chakula, malazi, mavazi n.k
Huku mwingine analipwa 15,000,000 huku akipewa mahitaji mengine bure.
Tofauti hapa ni majukumu.

Majukumu wise huwez mlipa mtu mshahara sawa.

Hakuna flat rate kwa mfumo uliopo
 
Habari!
Dar es salaam ina kanda kuu kama nne hivi, KANDA YA GONGOLAMBOTO na viunga vyake, KANDA YA MBAGARA na viunga vyake, KANDA YA MBEZI BEACH na viunga vyake na KANDA YA MBEZI LOUIS/KIMARA na viunga vyake.
Serikali ijenge barabara katika kanda hizi.
Barabara ziwe za kulipia angalau 2000-5000 kwa gari binafsi na 5000-10000 kwa gari za abiria.
Hizi barabara ziwe na vituo vichache tu na speed ni kuanzia 80 km/h - 120 km/h. Chini ya speed hiyo ni faini.
Hapo mtu utaweza kuondoka Tegeta saa moja na nusu na kufika kazini Posta saa mbili kamili
Tafadhali Watu wa DCEA ongezeni bidii yenu katika Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kulevya ( Bangi na Gongo vikiwemo ) kwa Watanzania kwani ni kama vile Watumiaji na Wahanga wanaongezeka kwa Kasi hata humu Mitandaoni.
 
Back
Top Bottom