Serikali ijenge hospitali yake ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, iachane na Bugando

Serikali ijenge hospitali yake ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, iachane na Bugando

kwani hospitali za serikali hazipo? kila
mkoa una hospitali ya serikali ya rufaa nafikiri, swali ni kwamba kwa nini wananchi wanachagua kutibiwa hospitali za kidini badala ya serikali? ulipaswa uanzie hapo, binafsi sioni sababu ya ugomvi zote za kidini na za serikali ziko kuhudumia wananchi na zote serikali ina jukumu ya kuhakikisha zinafanikiwa ila mkianza hizi vs zile waumiao ni wananchi kwani nina uhakika wewe ukiugua utapelekwa nnje na serikali kutibiwa, lkn wengi wanaohudumiwa na hizi hospitali za kidini “hawajabarikiwa” kama wewe, hizi huduma ktk taasisi za kidini zipo sehemu remote ambapo hata serikali ni kama haipo …
Mwanza hakuna
 
Wala DDH ya Bunda sio ya wakatoliki, ni ya Wamenonite. Ukimwambia mgonjwa kati ya hospitali ya serikali na DDH na hospitali ya serikali mgonjwa ataenda DDH. Serengeti, Rorya hospitali zote kuu ni za makanisa na taasisi za dini.

Mwanza ukimwambia mgonjwa aende kati ya Sseke Toure ama Bugando mgonjwa ataenda Bugando. Same na hospitali zote za kidini zilizopo nchi nzima.

Hakuna mahala popote Duniani serikali inaweza kufanya kila kitu, serikali inatakiwa kushirikiana na sekta binafsi.

KAma hutaki hospitali pia usitake mashule, vyuo vikuu na huduma zote zinazotolewa na taasisi za kidini.
Bunda DDH ni KKT
 
Nashauri serikali owe na mpango wa muda mrefu wa kujenga hospitali yake ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, iachane na Bugando ambayo si mali yake, na wenye mali wanapnekana kunyanyapaa serikali.

Hii imefanyika maeneo kadhaa kwa kuondoa District Designated Hospital za makanisa na kujenga za kwake, mfano Wilaya ya Bunda.

Makanisa yaanze kujipanga kujitegemea kuendesha taasisi za, sio kutegemea serikali..... JPM mkatoliki alianza kuliona hili mapema na aliwapasha maaskofu wakapashik. Maana walimfata ili asitishe mpango huo wa serikali.

Pia serikali ijenge Chuo Kikuu Mwanza na mahala penguins, maana hawa wakatoliki wamekuwa wakiomba serikali isijenge vyuo vikuu mwanza kwa kuhofia ushindani kwa chuo chao cha SAUT
Tatizo la afya ya akili linakuwa kwa kasi sana ulimwenguni. Bahati mbaya zaidi wagonjwa wengi hawafahamu kuwa tayari wameshafika hatua mbaya sana ya ugonjwa
 
Nakuunga mkono kwa asilimia 100. Bugando ni janga. Mgonjwa mahututi analetwa kwa rufaa toka aidha Tarime, Bunda, Serengeti au Musoma na akifika mapokezi anakaa pale kwa masaa matano bila tiba/huduma yeyote. Mwishowe huyu mgonjwa mahututi anaaga dunia bila tiba yeyote. Serikali iunde Tume kwa ajili ya Bugando na ije na suluhisho la kudumu.
 
Kama unazungumzia ijenge hospitali ya Rufaa ya KANDA sawa.

Hospital ya rufaa ya mkoa wa Mwanza ni Sekou Toure.
 
Nakuunga mkono kwa asilimia 100. Bugando ni janga. Mgonjwa mahututi analetwa kwa rufaa toka aidha Tarime, Bunda, Serengeti au Musoma na akifika mapokezi anakaa pale kwa masaa matano bila tiba/huduma yeyote. Mwishowe huyu mgonjwa mahututi anaaga dunia bila tiba yeyote. Serikali iunde Tume kwa ajili ya Bugando na ije na suluhisho la kudumu.
Are you normal?
 
Kuna hospitali ya Sekoutoure. Ikiboreshwa zaidi inaweza kufikia standard za Bugando. Wanatakiwa kuongeza Bed Capacity na Specialized services.

Pia suala la Chuo kikuu ni muhimu, Mwanza ni Jiji kubwa Sana kukosa Chuo kikuu Cha serikali.
 
Ndugu mleta mada hivi Kati ya kanisa na serikali Nani alianza kumuhitaji mwenzake ili kufanya KAZI pamoja mbona unaongea as if Kanisa lilikuwa halijiwezi hivyo liliomba serikali iingilie Kati?? Ukisema hivyo kama unavyosema basi ujue ni taasisi/majengo mengi itabidi zirudi Kwa Kanisa.
 
Nashauri serikali owe na mpango wa muda mrefu wa kujenga hospitali yake ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, iachane na Bugando ambayo si mali yake, na wenye mali wanapnekana kunyanyapaa serikali.

Hii imefanyika maeneo kadhaa kwa kuondoa District Designated Hospital za makanisa na kujenga za kwake, mfano Wilaya ya Bunda.

Makanisa yaanze kujipanga kujitegemea kuendesha taasisi za, sio kutegemea serikali..... JPM mkatoliki alianza kuliona hili mapema na aliwapasha maaskofu wakapashik. Maana walimfata ili asitishe mpango huo wa serikali.

Pia serikali ijenge Chuo Kikuu Mwanza na mahala penguins, maana hawa wakatoliki wamekuwa wakiomba serikali isijenge vyuo vikuu mwanza kwa kuhofia ushindani kwa chuo chao cha SAUT
wafanye haraka ili watupunguzie foleni
 
Back
Top Bottom