Kwani ni ajabu ? Je haiwezekani ? Kwa nini mnafuta probability ?
Raisi aliekuwepo Waziri Mkuu basi wote walituambia uongo ? Kabla zilikuwepo tetesi kuwa Raisi Marehemu Magufuli ni mgonjwa au sivyo ? Wakajitokeza viongozi kuwa sio kweli Magu ni mzima na anawapa salamu ?
Hivyo habari zipo ndio zipo na kama ni kosa basi waliosema Rais ni mzima ndio walioteleza na kukosea ? Mbona maalim Seif alitangaziwa tokea alipopata covidi hadi akapata nafuu hadi alipozidiwa nae haikuwa salama ikavuma ameuliwa,kwani alipata hujambo ,sasa huyu tuliambiwa mzima ghafla bin voom tukatangaziwa amefariki.
Angalizo viongozi wanapooumwa hata na ukucha ni bora mtangaze na wananchi na wadau wa dua baelewe na kuomba.
Walioficha habari ndio waliomuuwa Mheshimiwa Magufuli maana hawakutaka aombewe dua. DUA ya mtu mmoja tu ingevuka vigingi na kukubaliwa basi Magu tungekuwa nae leo,lakini mlitulisha uwongo kuwa Magu ni mzima na anachapa kazi,wajibikeni kwa kutulisha matango pori,ndio uungwana au mtupe sababu za kwa nini mlisema uwongo au iliwabidi mseme uwongo.
waandishi mnaokutana na viongozi wanaoita vyombo vya habari kila uchwao waulizeni ilikuwaje hapo.