Serikali ikemee kwa nguvu zote wanaodai Hayati Magufuli kauawa, iondoe video zote YouTube na kuwasaka wahusika

Naomba niongee hili toka rohoni na nitangulize kuomba radhi kwa watakaokwazika na hili andiko langu
Yeyote aliyehusika na kifo cha mwanakwenda awe pekeyake ama kikundi anastahili kupewa heshima kubwa na kutambuliwa kama shujaa wa Taifa...
Duuhh
 
Kila mtu ana haki ya kuamini anachokiamini na kutazama/kusikia anachopenda.
 
Sio tuu kukemea bali wakamatwe Ili wakatoe ushahidi ,kuwaachia wanaeneza ushenzi hao
 
K

Labda ni kweli.?Mama amesharuhusu Uhuru wa vyombo vya habari.Ww unakuja na ukandamizaji was habari.Hauoni kuwa haumtendei haki?Au ni ww unahusika nn?
Matumizi mabaya ya uhuru,freedom of speech ipo ila freedom after speech itategemea umeandika nini
 
Siku 4 au 3 kabla ya tarehe 17 mwezi wa 3.
Niliona mizinga ikiwa na wanajeshi inatoka bagamoyo inaelekea dar.
Nikamwambia mjomba hii mizinga inayopita sio Hali ya kawaida.
 
Causation................!!!!!!!

Duniani kuna siri basiiii, watu watasema tu.sema kama wapo wengine wanahofia kupoteza kibarua. Yetu macho
 
Haya sasa umeona kwanini hujampiga breki huyo au kwa sababu wewe na yeye wamoja?

Jifunzeni kuheshimu kila mmoja maoni yake usitangulize kukwazika au kuwatishia wengine hapo unategemea hao wanaolalamika watapikwa chungu kimoja na huyo aliyekushangaza kwa kauli yake hiyo?
 
Huyu kafa kwa mfumo wa umeme wa Moyo Pacemaker basi. Hayo mengine unalazimisha wewe. Hakuna Mtu duniani aliwahi kuishi na kifaa Cha pacemaker kwa zaidi ya miaka 10. Kama yupo tupe jina lake na nchi yake.
Wewe unaongea nini? Sasa hivi zipo mpaka za 15yrs bila kubadilishwa.kama una dr wa moyo yupo nje ya nchi muulize utapata jibu
 
Huu ujingaujinga utaligawa Taifa, Kila siku habari mpya ya jinsi alivyouawa. Wanakera mno watu hawa. Ajabu Rais alisema atawakamata, ajabu hawakamatwi.
Wakamatwe na wa chadema wanosema uongo kila siku.
Mtuhumiwa namba moja ni Lema ambaye alianza kutabili kifo na wa pili ni tundu kisu hao waje waksaidie upelelezi
 
Huyo fisadi alikufa kwa matatizo yake binafsi
 
Video hizo ziendelee kuonyeshwa youtube na mitandao yote, mimi sioni shida watu kutuhabarisha, kwani kuna hofu gani kwenye hizo video hadi zifutwe?
 
Wewe unaongea nini? Sasa hivi zipo mpaka za 15yrs bila kubadilishwa.kama una dr wa moyo yupo nje ya nchi muulize utapata jibu
Magufuli aliwekewa ya miaka 10 mwaka 2011 Enzi hizo ndiyo za muda mrefu. Umenielewa?
 
Kwani ni ajabu ? Je haiwezekani ? Kwa nini mnafuta probability ?
Raisi aliekuwepo Waziri Mkuu basi wote walituambia uongo ? Kabla zilikuwepo tetesi kuwa Raisi Marehemu Magufuli ni mgonjwa au sivyo ? Wakajitokeza viongozi kuwa sio kweli Magu ni mzima na anawapa salamu ?
Hivyo habari zipo ndio zipo na kama ni kosa basi waliosema Rais ni mzima ndio walioteleza na kukosea ? Mbona maalim Seif alitangaziwa tokea alipopata covidi hadi akapata nafuu hadi alipozidiwa nae haikuwa salama ikavuma ameuliwa,kwani alipata hujambo ,sasa huyu tuliambiwa mzima ghafla bin voom tukatangaziwa amefariki.
Angalizo viongozi wanapooumwa hata na ukucha ni bora mtangaze na wananchi na wadau wa dua baelewe na kuomba.
Walioficha habari ndio waliomuuwa Mheshimiwa Magufuli maana hawakutaka aombewe dua. DUA ya mtu mmoja tu ingevuka vigingi na kukubaliwa basi Magu tungekuwa nae leo,lakini mlitulisha uwongo kuwa Magu ni mzima na anachapa kazi,wajibikeni kwa kutulisha matango pori,ndio uungwana au mtupe sababu za kwa nini mlisema uwongo au iliwabidi mseme uwongo.

waandishi mnaokutana na viongozi wanaoita vyombo vya habari kila uchwao waulizeni ilikuwaje hapo.
 
Makubwa yapi kutunyima Ajira? Bora Amekufa kwakweli
 
Huyo kaburi lake alijichimbia mwenyewe, huwezi kuwafanya wananchi karibu milioni 60 wawe mateka wako na bado utegemee kubaki salama.

Pia mataifa yenye nguvu duniani kutwa nzima unakaa kuwandia tu eti mabeberu, mabeberu huku wamewahi kuwaondosha hapa duniani watawala waliokuwa na nguvu kukuzidi mbali sana. Lazima uwe umekalia kuti kavu.
 
Alikuwa akiombewa Kila siku, hata yeye mwenyewe alikuwa atikumbusha tumwombee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…