DOKEZO Serikali iliangalie hili la uuzwaji vyakula mtaani bila vibali maalum; kuna hatari kubwa mbeleni

DOKEZO Serikali iliangalie hili la uuzwaji vyakula mtaani bila vibali maalum; kuna hatari kubwa mbeleni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nyama choma ya kuku na ng'ombe zimekuwa biashara iliyoshamiri hasa katika vituo mbalimbali vya daladala hasa jijini Dodoma na Dar es Salaam yaan mtu yeyote anaweka meza njiani na ndoo ndogo iliyojaa nyama anaanza kuuzia raia vitu kama mishikaki ya mia mbili, miguu ya kuku, vichwa vya kuku na wakati mwingine na vipande vikubwa vikubwa vya kuku au ng'ombe.

Mimi binafsi nasema baadhi ya nyama hizi sio salama kabisa kwani mpaka sasa nnavyoongea nmepata shida ya ngozi baada ya kununua vipande vya kuku; Baada tu ya kutumia nyama hizo nimekuwa nilisumbuliwa na kutokwa na vipele vidogovidogo vinavyowasha sana maeneo yenye maungio ya mwili (yaan joints) baada ya kutumia dawa niliendelea vizuri ila nikafanya jaribio la kununua kuku sehemu nyingine ili nione kama nina allergy na kuku lakini sikupata shida. Nikanunua tena kuku sehemu ileile (ambayo mwanzo niliyonunua) ila nilipokula shida ile ikajirudia tena.

Naomba serikali itoe utaratibu na ukaguzi mkubwa sana kwa wauzaji wa vyakula vya haraka(yaan fast food) hasa maeneo ya stendi na maeneo yenye mikusanyiko ya watu hii ni hatari kubwa sana kwa wananchi na hasa watoto maana huvutuwa sana na vitu vidogovidogo.
 
Maoni Yako yasipuuzwe chakula ni kitu sensitive mno!
Ni suala la kuwa na mamlaka (bwana afya)atakae kuwa anathibitisha usalama wa chakula na mazingira
 
Back
Top Bottom