Serikali ilimzuia Julius Nyerere asiendelee kufanya kampeni za TANU

Serikali ilimzuia Julius Nyerere asiendelee kufanya kampeni za TANU

Mdanganywa

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
620
Reaction score
343
Mwaka 1957 chama cha TANU kilishaonekana ni tishio kwa serikali. Serikali ikaanza kukabiliana nacho.

Serikali ikasema kwamba Rais wa TANU yaani Julius Nyerere anatukana viongozi wa serikali. Hivyo chama cha TANU ni chama cha wakorofi kinachovunja amani ya nchi.

Hivyo Serikali ikaanza kufunga matawi ya TANU mfano tawi la Tanga likafungwa

Baadaye serikali ikazuia TANU kufanya mkutano wowote wa hadhara. Hivyo kipindi kirefu cha mwaka 1957 ikawa TANU imezuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

Jadili, fananisha, tabiri
 
Serikali zote zinazogandamiza watu, wale wanaogandamizwa wanapotaka kujikomboa, cha kwanza Serikali hizo hutunga sheria nyingi za hovyo kama zile mitandao na za kudhibiti shughuli za kisiasa na uhuru wa vyombo habari.

Serikali ya Magufuli ilianza na hayo hayo. Kwa muda mfupi ilitunga sheria:

1) sheria ya kuminya uhuru wa vyombo vya habari

2) sheria ya kudhibiti takwimu

3) sheria ya kudhibiti mitandao

4) shwria ya kudhibiti shughuli za vyama vya kisiasa

Haya ndiyo waliyofanya:

1) serikali ya kaburu mbaguzi Botha wa South Afrika

2) serikali ya Gadafi wa Libya

3) serikali ya dikteta Mabuto wa Zaire

4) serikali ya dikteta Nguema wa Afrika ya Kati

5) serikali ya dikteta Pinochet wa Chile

6) serikali ya dikteta Nicholaus wa Romania

Lakini wananchi wa mataifa hayo walizipuuza sheria hizo za kidikteta na mwishowe walishinda.

Inachofanya Serikali ya Awamu ya 5 siyo kipya, wanaiga yaliyokwishafanywa, na kwa vyovyote wananchi wa Tanzania watashinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiizi ni tabia za kikoloni kuwazuia wengine wasishikriki siasa.
Tazama kule palestina jinsi mayahudi wanavyowazuia Wapalestina kutetea haki zao.
Tazama Tanzania Inavyojionesha ina demokrasia kwa upande mmoja na inainyakua kwa upande wa pili Chini ya CCM.
 
Back
Top Bottom