Serikali zote zinazogandamiza watu, wale wanaogandamizwa wanapotaka kujikomboa, cha kwanza Serikali hizo hutunga sheria nyingi za hovyo kama zile mitandao na za kudhibiti shughuli za kisiasa na uhuru wa vyombo habari.
Serikali ya Magufuli ilianza na hayo hayo. Kwa muda mfupi ilitunga sheria:
1) sheria ya kuminya uhuru wa vyombo vya habari
2) sheria ya kudhibiti takwimu
3) sheria ya kudhibiti mitandao
4) shwria ya kudhibiti shughuli za vyama vya kisiasa
Haya ndiyo waliyofanya:
1) serikali ya kaburu mbaguzi Botha wa South Afrika
2) serikali ya Gadafi wa Libya
3) serikali ya dikteta Mabuto wa Zaire
4) serikali ya dikteta Nguema wa Afrika ya Kati
5) serikali ya dikteta Pinochet wa Chile
6) serikali ya dikteta Nicholaus wa Romania
Lakini wananchi wa mataifa hayo walizipuuza sheria hizo za kidikteta na mwishowe walishinda.
Inachofanya Serikali ya Awamu ya 5 siyo kipya, wanaiga yaliyokwishafanywa, na kwa vyovyote wananchi wa Tanzania watashinda.
Sent using
Jamii Forums mobile app