A
Anonymous
Guest
Kama sikosei, mwaka huu 2026 Serikali ilitoa utaratibu wa kuwaruhusu wafanyabiashara wapya kufanya biashara kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kutozwa kodi, ikiwa wamejisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN), na suala hilo lilipitishwa na Bunge.
Swali langu ni moja: kwa nini bado baadhi ya maafisa wa TRA wanapofika kwenye biashara mpya wanaonekana kuwa na ugumu kuelewa utaratibu huo hata baada ya wafanyabiashara kutoa maelezo?
Je, ni kweli kuwa wafanyabiashara wapya wamepewa msamaha huo, na kama ndivyo, ni aina gani za biashara zinazohusika na utaratibu huo ili wafanyabiashara waweze kufahamu vizuri?
Au je, sheria hiyo bado haijaanza kutumika rasmi? Ni muhimu kupata ufafanuzi ili kuepusha mkanganyiko kati ya wafanyabiashara na mamlaka husika.
Ufafanuzi wa Mamlaka, soma ~ TRA: Wafanyabiashara wapya waendelee kujiachia mwaka mzima, wana msamaha wa kodi