Shida ya serikali ya hii nchi ni kukurupuka na kutokuwa na mipango. Walipaswa kuandaa walimu kisha ndio waanzishe hayo masomo mapya. Ila wao walikurupuka wakaanzisha masomo ambayo hayana walimu. Hivyo kuzima moto ndio ikabidi waajiriwe wasio walimu kuokoa jahazi. Nakumbuka mtoto wa mjomba wangu akilalamika shuleni kwao wanatakiwa kusoma kompyuta na somo la biashara na hakuna walimu na hapo ilikuwa June. Sijui hata kama waliyasoma hayo masomo au la!