Yaani nyie watu mna matatizo sana!!! Yaani mnataka alichosema JPM kisikosolewe na ukimkosoa basi una chuki nae!!!
Anyway, mimi ni miongoni mwa hao watu tunaoambiwa TUNA CHUKI na Marehemu kwa sababu tu huwa napenda kuweka kumbukumbu sawa!!
The Hater Pro narudia tena hapa...
Popote pale duniani kodi ni Mali ya Serikali kwahiyo mambo ya kutokusanya kodi SIO YA KWELI...
Hata hivyo, ni kweli zipo BAADHI ya kodi zinazoweza KUSAMEHEWA kwa mujibu wa sheria zetu wenyewe!!! On top of that, binafsi nilihusika kwenye research kuhusu Belt and Road Initiative (BRI) iliyoasisiwa na China!! BRI ndiyo imezaa miradi kadhaa ya Uchina sehemu mbalimbali duniani!
Wapinzani wakubwa wa BRI ilikuwa Serikali ya Trump ambayo iliwaaminisha hadi Wamarekani wenyewe kuhusu ni namna gani BRI inavyoandaa MSIBA kwa nchi maskini! Propaganda walizokuwa wanasambaza ni pamoja na:-
1. Hizo Bandari zinazojengwa na China ni Mtego wa Madeni, na hivi sasa China wameipokonya Sri Lanka bandari yake baada ya Sri Lanka kushindwa kulipa madeni
2. Uchina inataka kuweka vituo vya kijeshi na hivyo usalama wa mataifa ya Afrika yapo hatarini kiusalama!
Media kadhaa za USA zikawa ndo wasambazaji wakubwa wa hizo propaganda!!
Baadae Wasomi wa huko huko Marekani wakashtuka na kujiuliza kama hii BRI ni mbaya kiasi hicho mbona mataifa kadhaa yanajiunga! Ili kupata majibu, ndipo baadhi ya taasisi ikiwamo Harvard University ikatuma wasomi wao kufanya research!! Kwenye hizo researches, ndipo nami nikabahatika kuwa "mbeba mikoba" wa Researcher Mmoja wapo kwa sababu yeye Case Study yake ilikuwa Bagamoyo Port Project, Hambantota Port (Maarufu kama Bandari ya Sri Lanka), pamoja na Piraeus Port ya Ugiriki!
Researcher wangu huyu, pamoja na wale wa Harvard University wakagundua yafuatayo kama yalivyokuwa summarized kwenye Abstract ambayo inapatika kwenye website ya
Harvard University!
View attachment 2086214
Binafsi nina full report sema sijapata muda wa kui-summarize na kuileta JF. Na utaona hapo juu Researchers ni pamoja na Deborah Brautigam and Meg Rithmire. Google mwenyewe hayo majina upate CV zao!!
Baada ya miezi kadhaa kupita tangu kukamilika kwa Research ya Bagamoyo, nikaona stori za kwamba hatukusanyi kodi zimekuwa nyingi mno! Ikabidi nimtumie email yule researcher niliyekuwa nae ili anifafanulie hili suala kwa sababu kwa sababu kwavile mwenzangu ni Mzungu, yeye aliweza kuongea na watu wa ndani zaidi.
Jibu ambalo alinirudishia, pamoja na mambo mengine ni hili hapa chini...
View attachment 2086237
Kwenye posts zangu za nyuma nishaandika sana kuhusu kama kodi itachukuliwa na serikali, sasa hao China watarudisha vipi pesa zao! Pamoja na njia nyingine za kurudisha, kama alivyosema Mwamba hapo juu, China, like many other businesses huwa WANAOMBA WASAMEHEWE INCOME TAX.
Narudia... WANAOMBA>>>> INCOME TAX! Income Tax ni sehemu tu ya Kodi zinazokusanywa bandarini! Ukisikia watu wanalalamika kwamba Kodi Bandarini inaumiza sana basi kodi hiyo wala sio Income Tax bali Excise Duty, Import Tax na VAT ambazo ZINAENDA serikalini!!
Hii Income Tax ambayo huwa wanaomba wasamehewe ni ipi?!
Kwa mfano, pale bandarini meli zitakuwa zinatia nanga, na watalipia USHURU (sio Kodi) wa wao kutia nanga bandarini! Kuna wengine watachelewa kuchukua au kusafirisha mizigo yao na kwahiyo itabidi ihifadhiwe hapo bandarini! Ni Wachina ndio watakaofanya kazi za KUPAKI NA KUPAKUA mizigo kwenye meli!!!
Sasa shughulizi zote nilizotaja hapo juu, na zingine kama hizo, zitakuwa zinawapatia Wachina Mapato a.k.a INCOME!! Kwa sheria zetu, Mchina atatakiwa kulipa Income Tax kutoka kwenye mapato anayoingiza kupitia hizo shughuli hapo juu!! Sasa basi, Wachina ndo huwa wana kawaida ya KUOMBA kusamehewa hiyo Income Tax! Kwamba, wakishusha na kupakia kontena kwenye meli, basi ile pesa watakayolipwa kwa hiyo huduma wanataka wachukue yote badala ya kulipia kodi!!
Kinyume chake, wewe ukiingiza let's kontena 100 kwenye bandari, KODI ZOTE utazilipa TRA kwa sababu ni MALI YA SERIKALI!!