Serikali imeishiwa haina pesa za mishahara

Serikali imeishiwa haina pesa za mishahara

Kama kuna ujinga mkubwa uliowahi kufanywa na Serikali hii ya Muungwana ni kupangia kima cha mishahara wenye sekta binafsi.
Siku niliposikia kimacha chini kikitangazwa tu basi nilijawa na wasi wasi kwa WaTanzania wengi kupoteza ajira.
Ukizingatia mauzo katika sekta hizo ni duni na bidhaa zake hulundikana kwenye maghala zikisababisha faida ndogo kuliko matumizi.
Serikali imetaka ionekane inawajali wananchi wake,kwa kupanga mishahara kwenye anga isizo husika nazo wala isizozifahamu sekta hizo zinapata faida gani,walichokifanya ni kupanga mishahara mikubwa isiyoweza kulipika.
Kwa ufupi mwenye sekta binafsi atalazimika kupunguza wafanyakazi au kufunga biashara zake na kuzihamishia nchi nyengine.
Naona hili suala lingeachiwa wenye sekta binafsi na wafanyakazi walitafutie kiwango cha kuwalipa wafanyakazi wao.
Naomba kuwasilisha hoja.
 
Serikali ilitafutie dawa sahihi tatizo la mishahara
VIWANGO vipya vya mishahara ya wafanyakazi ambavyo vilitakiwa kuanza kutumika kuanzia mwezi uliopita (Januari) vimezua vurugu baina ya wafanyakazi na waajiri.

Sababu kubwa ya vurugu hizo ni kufuatia baadhi ya waajiri kutokuwa tayari kulipa viwango vipya vya mishahara, baada ya serikali kuridhia maombi yao (waajiri)yaliyokuwa yameambatana na sharti la kwamba kama wakilipa viwango vipya basi waruhusiwe kupunguza wafanyakazi.


Sekta iliyokumbwa zaidi na mkasa huo ni viwanda, ambayo wafanyakazi wake waligoma kupokea mishahara ya zamani ya Sh80,000 kwa kima cha chini wakidai kuwa lazima wapewe kiwango kipya cha Sh150, 000 kwa mwezi kilichowekwa na serikali.


Juzi ilikuwa siku ya kulipwa mishahara, wafanyakazi wa baadhi ya viwanda vikiwamo vya Sunflag cha Arusha, Urafiki na cha Mabomba vilivyoko eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam waligoma kupokea mishahara yao pamoja na kufanya kazi mpaka watakapolipwa kiwango halali kilichotangazwa na serikali.


Mbali na kugoma huko, baadhi ya wafanyakazi waliamua kwenda kumvamia na kumtoa ofisini Afisa Utumishi wa Kiwanda cha Urafiki kwa madai kwamba yeye ni chanzo cha wao kutolipwa mishahara mipya.


Mbaya zaidi wafanyakazi wa Kiwanda cha Sunflag walifikia hatua ya kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima aliyekuwa akiwasihi wakubali kulipwa kiasi hicho wakati suala lao likiendelea kushughulikiwa.


Kufuatia vurugu hizo zilizoambatana na kuimba nyimbo za kuwakejeli viongozi wa kiwanda na serikali pamoja na kukataa kutoka kwenye eneo la kiwanda hicho, Polisi wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) waliitwa na kuwatawanya kwa kuwapiga mabomu ya machozi na virungu.


Hakuna anayefurahishwa na vitendo vya wafanyakazi kugoma, lakini nani wa kulaumiwa katika suala hili ambalo amri na agizo la utekelezaji wake unaonyesha kuwa ulichukuliwa bila kufanya utafiti wa kina?


Katika hili wafanyakazi wanaweza kuonekana na waajiri wao kuwa ni wakorofi na wakati huo huo waajiri kuonekana kuwa wadhalimu wakubwa wasiojali haki za watu wanaowatumikisha katika kazi zao.


Lakini kwa namna moja au nyingine serikali nayo inawajibika kwa tatizo hilo kwa kuwa ndiyo iliyotoa uamuzi kwamba lazima wafanyakazi wa sekta hiyo walipwe kiasi cha Sh150,000 kwa mwezi kama kima cha chini bila kuafikiana na waajiri wa sekta hiyo.


Serikali ilitakiwa kwanza kuwashirikisha waajiri juu ya marekebisho ya mishahara ili kuondoa utata kama uliojitokeza sasa kabla ya kutangaza viwango vipya. Tunasema hivyo kwa sababu mara baada ya kutangazwa viwango hivyo waajiri walisema hawawezi kulipa kiwango hicho na kupendekeza kuwa watakubali kufanya hivyo kwa sharti la kupunguza wafanyakazi kwa karibu nusu ya waliopo ili viwanda vyao visipate hasara.


Kibaya zaidi, baada ya kutangaza kiwango hicho na waajiri kutamka kuwa watapunguza idadi ya wafanyakazi, serikali iliwabembeleza na kuwakubalia kushusha kiwango hadi Sh80,000 kimya kimya na baadaye kutangaza kupitia kwenye vyombo vya habari juu ya mabadiliko hayo ambayo hayakuwa wazi kwa wafanyakazi.


Hilo linaonyesha kuwa serikali haikuwashirikisha kikamilifu wadau wote, kwani ingefanya hivyo ingetangaza viwango ambavyo sasa vinaathiri uzalishaji viwandani na maslahi ya wafanyakazi pia.


Jana Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati akizungumza na Waandishi wa habari mjini Dodoma alirudia kuonya kuwa migomo kazini ni makosa na kwamba mtu yeyote atakayefanya hivyo anaweza kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.


Hata hivyo, hilo siyo jawabu la matatizo hayo, tunaomba serikali itafute ufumbuzi wa kudumu ili kuumaliza mtafaruku huo unaowaathiri waajiri na wafanyakazi.
 
Shukrani, asante sana mkuu kwa maandishi yako mazuri yanayoonyesha balance.
Source of problem hii ya mishahara ni ubabe wa Chiligati. Amevuruga sana sekta binafsi, lakini mimi nahisi ya kuwa hii haikuwa bure. Kumbuka suala hili la mishahara imekuja baada ya serikali kubanwa sana na vyama vya wafanyakazi kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa serikalini. Sasa wakaona ngoja tuwasukumie sekta binafsi lawama.
Ubabe wa huu serikali na populism ndiyo unaowaangusha. Hapa hakuna mjadala, Chiligati ni lazima ajiuzulu na serikali inabidi itangaze 'reconciliation' committee, ili wadau wote wahudhurie na kuwepo na uwazi kuhusu upangaji wa mishahara.
 
Susuviri,unajua maamuzi ya kukurupuka pasipo kufanya utafiti wa kina ndiyo ambayo yamekuwa yakiigharimu nchi hii. Hebu fikiria unaambiwa umlipe House girl 60,000/=, wakati huo mfanyakzi unapokea 80,000/=, inaingia akili hii kweli,hii inaonyesha jinsi watu wavyokurupuka kufanya kufanya maamuzi.
 
Hivi Chi ligati pale nyumbani kwake kweli anamlipa maid 80,000?

Hivi Bar Maids nao sheria imewapangia shs ngapi?

Hata kama hakuna biashara ni lazima walipwe hivi viwango vipya?
 
Mzalendo halisi,muulize huyu mpumbavu Chilligati,maana watu wanakurupuka tu na msimamo ya chama. Wakati fulani mwalimu alisema,hatuhitaji viongozi ambao wanatoa maamuzi baada ya kuambiwa na wake zao
 
Nimeona nijaribu kuwashawishi WaTanzania ambao bado inaonekana wapo nyuma kimaendeleo, wakati Inchi inapita kwenye mambo makubwa makubwa ya ufisadi bado kuna wengine nao huwazidishia umasikini wananchi kwa kuwaibia Mishahara.
Tatizo hili linaweza kuondolewa mara moja bila ya tabu yeyote na wizi wa aina hii kutoweka hapa Nchini.
Dawa ambayo nimeiona ni kwa yale mashirika ambayo idadi ya makusanyo ya mishahara itavuka kiwango cha Milioni moja ,hivyo kuiondowa mipango inayofanywa na baadhi ya wafanyakazi kuandaa mipango ya kuiteka mishahara ,kwani siri za lini na wapi na nani wanaenda kuchukua fedha ya mishahara inajulikana na wao wafanyakazi wajanja wakiwemo hata mameneja ambao baada ya wizi kukamilika nao hukatiwa donge.
La kufanywa ni jambo moja tu wafanyakazi wote ni lazima wafungue akiba ya benki katika mabenki yaliojaa hapa nchini mpaka vijijini ,hakuna sababu ya tajiri kuwalipa wafanyakazi fedha mikononi hayo ni mambo ya kikoloni kwa wafanya kazi wa kudumu katika nchi iliyojitawala.
Kampuni yeyote itakayojulikana kuwalipa fedha wananchi mikononi basi izuiliwe kufanya biashara mpaka imehakikisha wafanyakazi wake wamekuwa na kufungua hesabu katika mabenki,jambo ambalo litapelekea wafanyakazi kufuata mishahara yao benki kwa wakati , ziko namna ya kuwalipa wafanyakazi hayo ni mambo ya kibenki na hayana tabu yeyote mishahara ya wafanya kazi inakuwa inaingia kila zikaribiapo siku za mapokezi ya mishahara kwa wafanyakzi inategemea na tarehe waliyokubaliana kati ya mfanyakazi na muajiri wake.
Hiyo ndio dawa pekee muajiri kutofanya hivyo ni kusababisha wizi wa mishahara na pia kusababisha hatari kwa mfanyakazi anapokuwa amepokea fedha na anarudi nyumbani kwa kukumbana na vibaka na kumpora feza yote ,ila ikiwa mshahara atatiliwa benki basi hata akienda kuchukua fedha ataweza kujipangia namna ya kuchukua anaweza akachukua kwa kiasi cha matumizi yanayohitajika kila wiki au mwezi.
Au mnasemaje WATANZANIA WENZANGU ? Na hata mabenki yatashawishika kutoa mikopo kwa wananchi ambao mishahara yao inapitia benki na hivyo kuwezesha wananchi kutumia fedha za benki kwa kupata mikopo ambayo wanautaratibu wa kuilipa na kujenga imani kati ya mabenki na wananchi tukiondoka hapo basi hatua zingine zitakuwa nzuri kwa wananchi kufaidi mikopo.
 
suala La Mshahara Wa Rais Limevutia Mjadala Hapa Jamvini Hivi Karibuni. Inaelekea Hivi Sasa Hii Ni Siri Kubwa. Lakini Ikumbukwe Kwamba Hapo Awali, Orodha Ya Watumishi Wa Serikali Ilikuwa Ina Chapishwa Mara Mbili Kwa Mwaka. Orodha Hiyo Ilikua Ina Onyesha Elimu, Mshahara, Jinsia, Lini Alianza Kazi, Nk.

Sijui Kimetokea Nini Hata Mishahara Ya Watumishi Wa Umma Ikaanza Kuwa Siri. Naambatisha Ukurasa Wa Kwanza Wa "staff List" Ya Mwaka Moja Wapo Kwa Kuanzia Na Ofisi Ya Rais. Tazama Kiambatisho Chini.

Macinkus
 

Attachments

Tofauti ni kubwa sana kati ya kima cha juu na cha chini.

Kuichapisha itakuwa aibu!
 
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inafanya mipango ya kuwalipa mishahara askari wa vikosi vyake; Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (Magereza), Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Zimamoto kupitia benki, badala ya mpango uliopo hivi sasa wa kuwalipa fedha taslimu maofisini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga, hatua hii ina lengo la kuwaondolea askari hao matatizo yaliyojitokeza mara kwa mara hivi karibuni ya wizi wa fedha za mishahara katika ofisi hizo. Wimbi hili la wizi wa fedha za mishahara limeigharimu serikali mabilioni ya shilingi hivi karibuni.
Waziri ambaye alikuwa akijibu swali ndani ya Baraza la Wawakilishi, amesema askari wa vikosi hivyo vya SMZ watafunguliwa akaunti katika mabenki na mishahara yao itaingizwa katika akaunti zao moja kwa moja.
Kwa kweli hatua hii ya serikali ni nzuri na infaa kupongezwa, ingawa imekawia. Kwa kiasi fulani uamuzi huu unaweza kusaidia kudhibiti wizi ambao umeonekana kukithiri katika vikosi vya SMZ na kusababisha watu wengi kuuliza kuna nini katika vikosi hivi, hata vitendo vya wizi sasa kuonekana kama ni vya kawaida na vinavyokubalika?
Wiki chache zilizopita, wizi wa fedha za mishahara ulitokea katika Kikosi cha Zimamoto na Uokozi mjini Unguja, na iliarifiwa kuwa watu 17 walikamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi. Katika wizi huo fedha zilizoibwa zilikuwa ndani ya kasha kubwa ambalo halikuvunjwa
 
Nchi yoyote yenye kulipa cash mishahara basi ni nchi isiyo na Governor wa banki kuu muelewa, ndio yale tulio ambiwa na Alhaji Hassan Mwinyi kwamba kuna watu waliosoma , lakini hawajkuelemikia. na ni Nchi ya Mumiani.
Inacho takiwa kuanzia kesho mishahara yote ipitie Bank.
 
Hivi serikali iko wapi na marekebisho ya mishahara sekta binafsi mbona tume iliyopewa kazi hiyo muda wake umepita lakini kimya sisi wananchi tunaofanya kazi sekta binafsi tunaumia maana nauli ziko juu, chakula bei juu, wenye nyumba wameshapandisha kodi wakijua kuwa mishahara imeongezwa kumbe hakuna kitu, jamani tunaumia kwa kweli! Serikali hii iko wapi? Mbona naona hamna maisha bora kwa kila mtanzania ? Isipokuwa maisha bora kwa wawekezaji wa nje na mafisadi tuuu?
 
Wakati Rais Jakaya Kikwete aliyeahidi kuwa malipo ya mishahara mipya na marupurupu ya wafanyakazi wa serikali italipwa mwisho wa mwezi huu akiwa kwenye pipa kuelekea kwa bushi (ziara ya 6 huko ndani ya miaka miwili na nusu) taarifa kutoka jikoni ziandokeza kuwa mishahara ya mwezi huu kwa wafanyakazi wa serikali itatoka tarehe tano mwezi wa nane.Hakuna uhakika kama ni kila sekta ya serikali lakini uhakika wa hilo upo kuvihusu vyuo vya umma nchini.

Ofisi husika na masuala ya fedha zimeweka wazi kuwa hakijaeleweka na wamepokea taarifa kuwa ni mpaka tarehe tano.

Wakati hali ikiwa hivyo ikumbukwe kuwa TUCTA walitoa tamko kuwa maadhamano ya wafanyakazi yatasimama kwa muda mpaka tarehe tatu kama malipo hayajafanyika uanze.

Kwa hali ya kawaida watanzania wengi tunaishi kwa mishahara, sijui hali itakuwaje kwa wadanganyika ambao kila kukicha wanakabwa kabali.

Uchunguzi hata hivyo haujaweza kubaini kama waadhirika wa kuchelewa kwa mishahara watajumuisha wafanyakazi wa ikulu, wizara, waheshimiwa wabunge na wakubwa wengine wa serikali au ni walalamajalalani makabwela peke yao.

Tusisahau kuwa prezidenti yuko Washington.Kama ni kutaimu kaweza manake alijua kwa hali hii tu lazima mgomo utakuwepo.

Haya haya jamani, wale wa kukopa tuendelee kukopa na daladala tuzione anasa.

Hii ndiyo Bongo ya EPA
 
Last edited:
Unazungumzia mwaka gani? Hiyo tarehe kwa mwaka huu imeshapita tayari
 
Mzee wa gumzo are you sure of what you are saying?

Kwani mwenye nyumba wangu nimemwahidi kumlipa kodi ya miezi iliyobaki kumaliza mwaka huu 2008 Jumamosi tarehe 30/08/2008. Kama mshahara hauleweki utatoka lini itabidi nijipange upya jinsi ya kumweleza mwenye nyumba wangu. Kwani nimekuwa nikimpa menye nyumba wangu hadithi za leo, kesho hadi sasa ninaonekana mwanas.....

Hali hii kama itapita bila mshahara kutoka hadi tarehe nane nitakosa fursa ya kununua share za NMB ambazo mwisho wake ni tarehe 8/9/2008 saa kumi.
 
Wanategemea kurekebisha baadhi ya idara kwa mwezi wa tisa na baadaye Januari watarekebesha idara zingine chache. Hivyo hivyo hadi wamalize mwaka huu wa fedha wakirekebisha idara moja baada ya nyingine.

Mpango huu ni mzuri kwani unawagawa wafanyakazi wakose mshikamano katika kudai maslahi yao, na pia unawasubirisha wafanyakazi bila wao kuwa na jinsi nyingine ya kudai.
 
Katika Hali iliyokuwa inatarajiwa kabisa, serikali ya Mheshimiwa Kikwete haina pesa kwa sasa za kulipa mishahara ya wafanyakazi wake na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwa habari za uhakika wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wameandikiwa barua kuambiwa hakuna mishahara mpaka pale serikali itakapotuma pesa. Mwanzoni tuliambiwa hapa JF kulikuwa na uwezekano wa kuwalipa tarehe 5/9.2008 lakini sasa ni mpaka serikali itakapotuma pesa.

Kama hilo halitoshi vyuo vyote vya serikali ambavyo vilikuwa vifunguliwe mwishoni mwa mwezi wa 8 hafitafunguliwa mpaka tarehe 29/9/2008. Tayari wanafunzi wote wameshataarifiwa kuhusu kuahirishwa huku. Hii ni kutokana na bodi ya mikopo kutopatiwa fungu lake la mikopo mpaka sasa hivi.



Hivi hili la kusema pesa zote za EPA (karibia billioni 200) ziingizwe serikalini sio katika kujaribu kuficha kwamba serikali haina pesa kwa sasa?
 
Yote hii ni kwa sababu viongozi wana matanuz ya hali ya juu sana. Nchi imekwisha.
 
Back
Top Bottom