Natumia nafasi hii, kumshukuru kwa dhati, Rais Samia Suluhu kwa nia aliyoionyesha ya kusaidia na kuwekeza zaidi katika Sekta za Uzalishaji, ulipozindua Agenda 1030, wengi walidhani hayatotokea lakini umehakikisha mambo haya yanatokea"
Rais Samia Suluhu umezindua Mfumo wa Utoaji wa Ruzuku ya Mbolea, bei ya DAP sokoni ilikuwa Sh. 131,675 sasa itauzwa 70 000, Urea 124,714 itauzwa 70 000, CAN ambayo inauzwa 108 156 itauzwa 60 000, SA ambayo sokoni inauzwa 87 872 itauzwa 50 000"
Mbolea aina mbalimbali zinazotumika kupandia (NPKs) ambazo zina wastani wa Shilingi 122,695 wakulima watazinunua kwa Shilingi 70 000 kuanzia sasa.
Katika mfumo huu wa utoaji wa ruzuku, mbolea inapovalishwa mfuko inapewa namba maalumu, kila mfuko utakuwa na namba yake tofauti. Mawakala wote wamesajiliwa na kila wakala ana namba yake tofauti na katika duka la wakala itawekwa namba ya simu na jina la kampuni
Tumekubaliana na Vodacom Tanzania, CRDB na NMB Tanzania kutakuwa na madawati ya usajili pembeni ya maduka yanauza mbolea ili mkulima akifika asajiliwe, apewe namba na siku ya mwisho atachukuliwa alama ya kidole.
Mbolea inaponunuliwa sisi tunaweza kuiona katika mfumo wakati huo huo na namba maalamu za QR code haziwezi kutumika sehemu nyingine baada ya kutumiwa mara moja.
Kila mfuko mmoja wa mbolea utajulikana umenunuliwa na nani, umenunuliwa kiasi gani na mnunuzi anaishi wapi, haya yote tunaweza kuyafahamu kwa kutumia mfumo huu mpya.
Ili mkulima aweze kuzalisha kwa tija, anahitaji mbegu, pembejeo na mbolea. Tatizo lilikuwa gharama ya mbolea leo hii tunamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuchukua hatua ya pili ya kupunguza gharama za pembejeo
Sekta ya kilimo kwa ujumla wake inachangia wastani wa 25% ya Pato la Taifa na imeajiri zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania, maana yake watu wengi tunachangia kidogo. Njia pekee ya kutatua tatizo hili ni kuongeza tija.
Tumeanza mchakato wa usajili wa wakulima, tunaendelea na nawashukuru Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa kuwasimamia wakulima, tutaendelea kushirikiana.
Kwa mikakati hii Tanzania tutafika mbali kiuchumi.