Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ni sawa na kumuuliza Mtanzania ambaye angependa kuwa na uraia wa US kama amelezamishwa kuwa Mtanzania, rubbish.Kwani kuna mtu analazimishwa Kupeleka Watoto shule za Umma?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni sawa na kumuuliza Mtanzania ambaye angependa kuwa na uraia wa US kama amelezamishwa kuwa Mtanzania, rubbish.Kwani kuna mtu analazimishwa Kupeleka Watoto shule za Umma?
Serikali hii ni ya kipumbavu sana!Huu mtaala ni mzuri kuuangalia na kuusimulia lakini utekelezeaji wake ni mgumu na hauwezekani katika mazingira yetu
Walimu ambao sisi ndo wadau wakuu wa elimu hatukushirikishwa labda tusingekuwa hapa
1. Vitabu mpaka Leo mwaka unaenda KUISHA havipo mashuleni hasa kwa shule za msingi
2. Mtoto darasa la kwanza wa kisukuma aanze kusoma na miaka sita huku akiwa na masomo zaidi ya sita + somo la kiingereza ambapo walimu pia hamna yaani mpaka Sasa shule nyingi mtoto wa darasa la kwanza hajapata ujuzi uliokusudiwa
3. Mtoto darasa la tatu hakuna hardcopy za vitabu walimu wanaazimana simu maana hata consistency ya kugawa vishkwambi kwa walimu serikali imeshindwa Wala Haina budget ya hivo vishkwambi, katika shule nyingi saivi walimu wenye vishkwambi hawazidi watatu
Nashauri Kila mwaka wa Budget walimu wapewe vishkwambi vipya,
4. Kuna somo la coding linaloanza darasa la tatu huku likilenga Kuweka msingi kwa kucheza electronic game , ambalo hili somo ni ngumu kuwafikia walengwa(wanafunzi) maana hata hivo vifaa vya kuinstall hizo games hamna
5. Mazingira ya walimu hovyo ofisi zao kama stoo, vifaa wezeshi kwa walimu hamna, kamshahara kaduchu , maslahi mengine kwa walimu hamna yaani ni tabu tupu.
Kuna kundi kubwa la watoto litamaliza halina ujuzi kitu ambacho ni hatari kwa taifa , hatua za haraka na za makusudi zichukuliwe , hata upimaji wa mitihani hii inayokuja kupima watoto wetu kiwilaya ni ya hovyo hovyo tu , wakuu wa shule wanashindana namna ya kutengeneza matokeo Ili aonekane na afisa elimu kuwa anafaulisha
Wewe huna ubavu wa kukijuwa Kiswahili kuliko Waswahili.uache sio uwache, usituletee Kiswahili cha Kipemba hapa.
Kujuwa lugha ya pili na zaidi ni kupanua sana mawazo, kwa wenye kuelewa.Mtoto kuchagua somo mojawapo la lugha mfano kichina sijui kiarabu eti lianzie darasa la 3, hapo bado mtoto huyo darasa la 3 hajajua vizuri kiingereza, alafu unaanza kumfunza kiarabu au kichina, huyo mtoto darasa la 3 lazima atachangaya sana mambo katika ubongo wake, yaani their brain will be overloaded sanaaa, sielewi kwanini hizo lugha wame introduce katika New Curriculum, hakuna haja ya mtoto mdogo darasa la 3 ahangaike kusoma kichina au kiarabu, huku kingereza chenyewe kinampa shida, hapa Waziri wa Elimu hakuangalia kabisa ugumu wa jambo hili zito sana with respect na watoto wetu, kiingereza tu bado shida, unamwambia mtoto haya soma kichina pia au kiarabu chagua moja hapo, huyo mtoto atavurugikiwa kabisa.!!
Hii sio sawa…!! Lugha za watu hizi zisiwe lazima kusoma with exception ya English..!!