Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Tuliona walichofanya wabunge Dodoma; tumeona wanachofanya wanazuoni kutoka kwenye dini na fani mbalimbali nchini. Wanajadili mule mule alipopita Mzee Mbowe na Lissu, tofauti ni kwamba wanazuoni wanawapiga shule mawaziri wakati wabunge waliwapigia makofi mawaziri bila kuwapa maarifa mapya.
Hiki kinachoendelea ni fedheha kwa bunge na wabunge; kwamba pamoja na kupitisha kumbe wao siyo final bali kazi yao ilikuwa rubber stamp au kukamilisha ratiba.
Goma limekuwa gumu na endapo Mbowe na Safu yao wataingia uwanjani kwenye mikutano ya adhara kwa agenda hii upo uwezekano pakatokea mmomonyoko mkubwa na makundi kuhusu bandari.
Changamoto kubwa ya Watanzania ni wanafiki wazuri; wakiona unataka kusikia habari hoja fulani nao wanakupigia makofi ila moyoni wana ukweli na wewe ukijiongezea unagundua huna watu nyuma yako.
Magufuli alisifika ila waliokuwa wanamsifu angewaruhusi wapige kura ya siri angelalamika kaibiwa kura kwa sababu baada ya kuondoka tu watu walewale waliokuwa mgongoni mwake walijitokeza kumkataa.
Kama walimkataa hadharani akiwa ameondoka je, walimpigia kura sirini? Kwa kuwa alifahamu fika kwamba amewakosea Watanzani aidha akiwa na nia nzuri au mbaya ndipo akaona njia sahihi ni kuchafua uchaguzi.
Kwa mantiki hii, hakuna mwenye uhakika wa nani ambaye anamkubali kiongozi wa CCM sirini. Wote tumebaki kusikia uungwaji mkono wa majukwaani ila unapokuja sirini hakuna mwenye uhakika wa kutoboa. Hii inatokana na ukweli kwamba tumewaweka makovu Watanzania kwa muda mrefu kwa kuwaaminisha tunafanya uwekezaji wenye tija matokeo yake hakuna tija.
Kwa hatua za awali Mhe. Rais ameona walipokosea wasaidizi wake, amejifunza kwa ndani nini jamii inataka, amewasikia viongozi wa kijamii na imani wanasimamia nini, lakini amewasikia wale wasaidizi wake bungeni walichangia nini; obviously amebaini wanaompotosha na kumchonganisha na jamii siyo wapinzani bali wasaidizi wake.
Inatia hasira unapodhani una wataalam wazuri kisha unagundua kazi waliyofanya inapigwa vita na kila msomi; swali la kujiuliza, hao wasomi walioteuliwa kukusaidia wameelimika? Wana exposure au wapo kwa sababu wapo?
Naamini soon Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake watapisha ofisi kwa kilichotokea, vinginevyo ikibainika mkataba haukuwa shirikishi, pamoja na kiburi cha kibinadamu bora tuchelewe kufika kuliko tufike tukiwa siyo wamoja.
Padri Kutima ametueleza Somalia na Sudan, mimi nataka niongeze Loliondo na Tarime mgodini, je, tunadhani ni nia zote nzuri ni nia nzuri?