Tetesi: Serikali imeondoa Posho za Safari Mpya kimyakimya?

Tetesi: Serikali imeondoa Posho za Safari Mpya kimyakimya?

Ni Bora kwamba wameliona hili mapema. Ifikie sehemu hela za Serikali zisitumike hovyohovyo. Tuwe wazalendo jamani. Hivi kweli 250k, 220k watu wanaenda safari siku 10 , mamilioni. Wakati miundombinu yetu bado ikiwa duni kiasi hiki.
Mimi pia ni mnufaika wa nyongeza tena kwa asilimia 120 lakini moyoni nilikuwa nasononeka sana kuwaumiza watanzia wenzetu kwa kujipendelea kiasi hicho.

Kama Kuna hela nyingi kiasi hicho za kujilipa 250k kwa siku, kwa nini wasizipeleke kwenye Miradi ya Maendeleo kuliko kutumia hivyo kila siku Ughaibuni kukopa!! Sio fair kabisa!

Tusihangaikie kujipendelea, tuhangaikie Taifa kwa ujumla. View attachment 2301473
Watu kama nyinyi mko wachache nchi hii, Sasahivi tunakizazi kisichokuwa na uruma kwa mwenzie,watu wakipata madaraka wanaangalia family zao na matumbo yao tu,wanataka wanachokusanya wakigawanye chote,arafu waanze kuwaambia wananchi eti nchi yetu Uchumi mdogo mala Kasungura kadogo sana hakatosherezi kumbe wao wameisha vimbewa.R.i.p Magufuri wanyonge tutamkumbuka daima
 
Wewe kama ni mtumishi unastahili kuwajibishwa nyaraka kama hizi ni sirikali unazisambaza mitandaoni mkichukuliwa hatua mnaona serikali inawaonea.
Nilimwambia na mwingine juzi ila hawaelewi,nadhani Mtendaji wa TanRoads na TCRA wafuatilie aliye post..

Huu ni utovu wa Nidhamu, hiwezi Kuwa na mfanyakazi mpuuzi kama huyu..
 
Acha ujinga, serikali ilipandisha viwango vya Posho na kusema kwamba bajeti zibakie zile zile..

Sasa TanRoads wao Kwa bajeti yao ya utawala na usimamizi wameona haiwezi kukidhi hizo rate mpya ndio maana wamesitisha tena hiyo ni memo ya ndani..

Taasisi zingine ambazo zinaona bajeti zao zinaweza kuhimili watalipa kama kawaida..

Mfano taasisi nayofanyia Kazi mpaka sasa inatumika rates mpya unless kama itaamliwa vinginevyo.
Wewe ni mbumbumbu na mpumbavu sana!

Tanroads ni taasisi ya nchi gani?
 
Wewe kama ni mtumishi unastahili kuwajibishwa nyaraka kama hizi ni sirikali unazisambaza mitandaoni mkichukuliwa hatua mnaona serikali inawaonea.
Hiyo mbona ni public documents? Inatumika kwa wadau wote .. hakuna Siri hapo.
 
Sasa si wangepunguza idadi ya safari ?

Hao jamaa nao ni noma tu !

Wanataka kuwaharibia wenzao!
 
Hiyo mbona ni public documents? Inatumika kwa wadau wote .. hakuna Siri hapo.
Ingekua ni public document ingetangazwa magazetini na bila shaka huyu aliyepost ni mtumishi wa umma au kaipata kwa mtumishi wa umma .hii haikubaliki mimi kama raia mwema wa nchi hii namfuatilia huyu jamaa nione mwisho wake.
 
Wewe kama ni mtumishi unastahili kuwajibishwa nyaraka kama hizi ni sirikali unazisambaza mitandaoni mkichukuliwa hatua mnaona serikali inawaonea.
Hakupaswa kusambaza dokezo kama hiv.huyu hazingatii maadil ya utumish.kama upo huko tanrod wewe uchekiwe.unapata faida gan kuweka memos za ndan kama hiv
 
Wajinga wanakamua nchi bila Huruma!!!Yaaani wanakipiza jinsi walivyo Nyooshwa na Mwenda zake.
 
Back
Top Bottom