KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Matanzania hata waongeze sukari kg 1 iwe 10000 yanalialia mtandao yakija ishu ya chama tu kwenda yanga yamesahau matanzania yote mambumbumbu
Uko sahihi,sisi mambo ya kijinga ndiyo tunabishana sana,hasa mambo ya umbea umbea,wakiona mjadala unaendelea kuwa mkubwa huu wa Luku wataongea na Diamond au Harmonize aachie clip ya ngono,basi mjadala utahama
 
Watanznaia wote tutampa kura za ndiyo, Dr. SSH.
Hata mimi ambaye stampa kura ni mtanzania halisia wa asili. Na sababu zangu kubwa 1. kupora rasilimali za Tanganyika na kuwagawia waarabu;
2) kuwapendelea wazanzibari kwenye ugawanyo wa pesa.
3) kuruhusi wateule wake waibe na kufanya ufisadi bila bugdha.

Hivyo usiseme watanzania wote, sema wewe binafsi au wewe na familia yako kama una udikteta kwenye familia.
 
Hii ni kweli wakuu awali ukinunua umeme wa 10000 unapata unit 28... Ila kwa sasa unapata unit 22.4 ina maana kuna upungufu wa wa 5.6 ambayo ni sawasawa na 2000
 
Hakika CCM imechoka
Mkuu, CCM kama chama hakijachoka maana kina kanuni, miongozo na katiba mzuri tu; na vyote vipo hai na vina mambo nyenye tija kwa Taifa na wananchi wake. Tatizo kubwa ni lile AZIMIO LA ZANZIBAR ambalo lina waruhusu Watumishi wa Serikali hasa viongozi Wakuu, kuwa na vitega uchumi vyao binafsi, ruhusa hii inasababisha mgongano wa kiutendaji na maamuzi, hasa ya kibiashara kati ya Serikali na viongozi hao wa Serikali katika Maputo na kodi ya Serikari na ya viongozi binafsi; mfano (mimi kama Mkurugezi ama Waziri wa Nyumba, na nina Nyumba 50 za kupanga na sheria inanitaka kulipia kodi ya Serikali , basi nitapindisha sheria hoyo ya kodi na kuielekeza ama kuipindisha kanuni za kodi hiyo kulipwa na mpangaji AU kama nina vituo vya petrol nitapenda kuongeza bei ama kodi zake kuto kuzilipa yeye na kutumia mbinu za kiofisi kuelekeza kodi hizo kulipwa na Wananchi.
Kwa hali tuliyonayo sasa hivi, pamoja na kuwa na Taasisi ya Maadili ya Viongozi, ambayo haikuonyrsha Utendaji dhabiti ni wakati mwafaka wa kuli rudisha Azimio la Arusha, ili anaye taka kazi za Serikali afanye kazi za SERIKALI na si vinginevyo.
 
Nikiwa miongoni mwa wanaouchukia uongozi huu unaomlimbikizia kodi na tozo mwananchi mlala hoi,

Juzi tena CCM wameongeza petrol kwenye moto wa kifuu kwa kuongeza tozo ya luku kwa mlala hoi

Ni nani atampa kura kiongozi huyu?
Mkuu huyu huko kwao anapita bila kupingwa
 
IMG-20240702-WA0009.jpg
 
Hiyo siyo bei ya umeme, ni kodi ya jengo.

Kama unaishi nyumba ya kupanga na una mita ya peke yako maana yake unamlipia kodi mwenye nyumba.

Hawa mwisho wao hauko mbali, Mungu amewatia upofu hawataamini ikifika punda anapogoma.
Sasa, Kama ni Apartments Si Watakua Wanakusanya Nyingi! Maana kila Mita Inajitegemea
 
Wakuu tuanzishe mgomo tafadhali
Tarehe 10 mwezi huu mgomo nchi nzima kama ni kufa acha tufe, yaani ni kufa ama kupona. Hii nchi bila damu kumwagika haiwezi kunyooka kamwe
1. Maisha magumu
2. Kodi za kumkandamiza mwananchi kila kona.
3. Utawala wa ovyo, raisi hafai na watendakazi wake ovyo
4. Viongozi wapenda rushwa kuliko haki
Tumechoka maisha ya kuwanufaisha viongozi hatutaki kuwa na kiongozi yeyote tutajiongoza wenyewe. Free Nation
Unawajua wabongo lakini, yaani hata Serikali ifanye nini hakuna atakayesimama kuandamana, na hata wakiandamana ni bomu moja tu la machozi wote wanasambaa
 
Kwa sasa makato ya kodi unaponunua LUKU yameongezeka kutoka TZS 1,000 mpaka TZS 2,000.

Tunaomba maelezo kwanini gharama hizi zineongezeka? Kuna sababu gani ya kuendelea kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu ili hali mabwawa ya umeme yaliyotumia matrilioni ya kodi za wananchi yameshafunguliwa?

Je, kodi wanazotozwa wananchi bado hazitoshi? Je, mmeshindwa kutumia rasilimali zilizopo nchini, kuna madini, maliasili na vivutio mbalimbali vya utalii n.k pamoja na vyanzo hivi vya mapato, serikali imeshindwa kuwa bunifu na kutegemea tozo na kuendelea kunyonya na kufanya maisha ya watanzania yazidi kuwa magumu?

Hali hii itaendelea mpaka lini?


View: https://www.instagram.com/p/C86xFc6qUUU/?igsh=MXh0Z2VtbzRpMHpyaA==
 
Back
Top Bottom