Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hayo yamebainishwa na Waziri wa wa Madini Anthony Mavunde katika uzinduzi wa ripoti ya 14 ya Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema, kampuni zilionesha kuwa zililipa kiasi cha shilingi trillion 1.878
serikalini na kupelekea kuwepo na tofauti kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402 sawa na asilimia asilimia 0.021 ya mapato yote yaliyoripotiwa na Serikali.
Aidha, Mavunde ameelekeza, tofauti hiyo sh milioni 402 kufanyiwa uchambuzi wa kina ili kujua visababishi vilivyosababisha kutofautiana ili Kamati iweze kuzipa makampuni na serikali ushauri wa nini kifanyike ili tofauti hizo zisiendelee kujitokeza kwenye linganishi zitakazofuata.
Mavunde amesema, taarifa hizo ni pamoja na takwimu za uzalishaji na usafirishaji wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia (Production and export data), takwimu za ajira katika sekta ya uziduaji, michango ya kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibilities-CSR) na ushiriki wa wazawa katika sekta ya uziduaji ikijumuisha kutoa huduma kwenye kampuni za uziduaji (Local content).
Awali, akizungumza katika hafla hiyo,Mwenyekiti wa kamati ya TEITI, Ludovick Utouh amesema lengo la uzinduzi wa ripoti hiyo ni kuweka wazi kwa ajili ya wananchi na wadau mbalimbali ili waweze kutumia takwimu zilizomo kufanya mijadala ya kuboresha na kuongeza mchango wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia katika Pato la Taifa.
Nae, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo ameipongeza serikali kwa kutoa taarifa ya wazi ya ulinganisho wa mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji na kutumia fursa hiyo kuwataka watanzania waipitie na kuona namna ambavyo sekta hii ya uziduaji inavyochangia kukuza uchumi wa nchi na kuwataka pia wananchi kutumia taarifa hii kushauri na kutoa maoni yao.