Serikali Imesema inatekeleza Sheria ya Afya ya Jamii ambayo inamtaka mtoa maudhui, mada au matangazo yanayohusu afya kupata kibali

Serikali Imesema inatekeleza Sheria ya Afya ya Jamii ambayo inamtaka mtoa maudhui, mada au matangazo yanayohusu afya kupata kibali

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Screenshot 2026-05-19 at 11-41-22 Instagram.png

Serikali Imesema inatekeleza Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009 Kifungu Na.173 (1), ambacho kinamtaka mtoa maudhui, mada au matangazo yanayohusu afya ya jamii kupata kibali kutoka kwa waziri wa afya au ofisa aliyeidhinishwa na waziri.

Kauli hiyo imeolewa bungeni leo Na Naibu Waziri wa Afya, Dk Florence Samizi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai,Saasisha Mafuwe, aliyehoji serikali ina mpango gani wa kudhibiti watoa elimu ya afya na aina ya ulaji mtandaoni bila kuwa na taaluma inayotambulika jambo linalowachanganya wananchi.

“Serikali inatambua ongezeko la watu binafsi /wataalamu wanaotoa elimu au ushauri wa afya na lishe kupitia mitandao ya kijamii, hali inayoweza kupotosha na kuhatarisha afya za wananchi.

“Hii inatokana na kukua kwa uelewa wa masuala ya lishe, afya, utandawazi na ongezeko la vyombo vya kutolea habari,” amesema Naibu Waziri na kueleza kuwa kushindwa au kwenda kinyume na sheria hiyo mtoa maudhui/mada atachukuliwa hatua za kisheria.


Pia soma: Watengeneza maudhui yahusuyo bidhaa za vyakula waonywa kutengeneza au kusambaza maudhui yanayoweza kuathiri afya za watu
 
Hilo swali ata ungeulizwa wewe, lazima ungejibu hivyo; kama asingejibu hivyo mjadala ungekuwa mrefu.
 
Kibano kiongezwe kwa hao wapotoshaji..yaani kama yule Prof yule, Mungu anamuona
 
Back
Top Bottom