JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Zamani ilikuwa ukifika ofisi za TRA au TANESCO basi ni lazima ukutanane na watu wanaoitwa vishoka, nina uhakika kwa sasa watu hao wamesambaa kwenye ofisi nyingi tu.
Binafsi sijawahi kufanya kazi na hao watu kwa kuwa naelewa wapo nje ya mfumo wa ofisi husika, lakini nimeshashuhudia mara kadhaa watu wakiambiwa na maofisa wa ofisi husika kuwa ‘nenda hapo nje waone hao watu watakusaidia’.
Mimi nilishawahi kuambiwa upuuzi kama huo nikawasha moto mpaka ikabidi nihudumiwe fasta kwa kuwa nilionekana kama naleta kiwingu.
Watu hao nina uhakika wanashirikiana na maofisa wengi wa ofisi ili watu washirikiane nao, waongeze cha juu kwa faida yao wachache lakini wanajisahaulisha kuwa wanawaminya raia wa kawaida.
Inakera sana, hivi najiuliza Serikali imeshindwa kabisa kuondoka hao wanaoitwa vishoka au imeamua iache uwe kama mfumo rasmi kwa nje ya ofisi wa kujiongezea kipato kwa maofisa wao?
Zamani nilizoea mambo kama hayo kuwa ofisi za Serikali lakini siku hizi kuna baadhi ya ofisi japo ni chache nilizoona zina wapuuzi kama hao.