Serikali imeshindwa kuondoa vishoka katika ofisi zao au imeamua uwe mradi kamili wa wafanyakazi?

Serikali imeshindwa kuondoa vishoka katika ofisi zao au imeamua uwe mradi kamili wa wafanyakazi?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Zamani ilikuwa ukifika ofisi za TRA au TANESCO basi ni lazima ukutanane na watu wanaoitwa vishoka, nina uhakika kwa sasa watu hao wamesambaa kwenye ofisi nyingi tu.

Binafsi sijawahi kufanya kazi na hao watu kwa kuwa naelewa wapo nje ya mfumo wa ofisi husika, lakini nimeshashuhudia mara kadhaa watu wakiambiwa na maofisa wa ofisi husika kuwa ‘nenda hapo nje waone hao watu watakusaidia’.

Mimi nilishawahi kuambiwa upuuzi kama huo nikawasha moto mpaka ikabidi nihudumiwe fasta kwa kuwa nilionekana kama naleta kiwingu.
Watu hao nina uhakika wanashirikiana na maofisa wengi wa ofisi ili watu washirikiane nao, waongeze cha juu kwa faida yao wachache lakini wanajisahaulisha kuwa wanawaminya raia wa kawaida.

Inakera sana, hivi najiuliza Serikali imeshindwa kabisa kuondoka hao wanaoitwa vishoka au imeamua iache uwe kama mfumo rasmi kwa nje ya ofisi wa kujiongezea kipato kwa maofisa wao?

Zamani nilizoea mambo kama hayo kuwa ofisi za Serikali lakini siku hizi kuna baadhi ya ofisi japo ni chache nilizoona zina wapuuzi kama hao.
 
Mambo ya riziki kaka. Waachie wajipatie chochote kitu mtaani hakuna ajira. Uchache wa wafanyakazi kwenye taasisi ndo huleta vishoka kaka.
 
Ofisi zinazohusika na Ardhi ndio balaa, ni kama vile wao ndio wanaendesha ofisi hizo [emoji24][emoji24]

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kitu inaitwa vishoka, Hao ni watoa huduma wasio rasmi. Wakishakuwa rasmi ndo haohao tunawaita consultants/service providers.
mimi naona wakati mwingine huwa tunayataka wenyewe, unakuta taasisi flani inasema na imebandika matangazo huduma flani ni bure lakini unakuta mtu badala ya kuingia ndani ahudumiwe anakubali kuhudumiwa na watu nje na anaambiwa lipia kiasi flani akijua kabisa ni bure.wengine ni kwa kutaka kutokaa hata dakika foleni ndiyo hivo tena wanajikuta wanapigwa pesa.mbona benki sijasikia kuna vishoka? au polisi mbona sijasikia kuna vishoka? mimi kuna siku kishoka mmoja alitaka niingiza mjini uzuri najua taratibu ilikuwa ofisi moja ya tra kaniambia tin namba 20,000 nikakubali kumbe nilitaka aingie ndani niwaite wale suma jkt walikuwa wapo ndani wanalinda. akastuka akakimbia.tusikubali waendekeza hawa ndiyo wanafanya huduma zionekane hakuna kumbe wanatengeneza mazingira.
 
Wako wengi sana kwenye ofisi za TRA, Serikali iwatambue, iwasajiri kisha iwaajiri kama watoa huduma kwenye Kila ofisi wanakopatia riziki. Wamejitengenezea mfuko ambao ni wa hiali, kwa namna moja wanapunguza mahangaiko kwa wateja. Ukiiamua kuwakwepa uwe umejipanga kuchezeshwa nenda rudi.
 
Machaka ya rushwa hayo, mambo ya kufanya ofisi za umaa kama vijiwe kamwe hayana tija.kama Kuna kiongozi WA ofisi ya serikali naruhusu mambo kama hayo hakika hatoshi
 
Wako wengi sana kwenye ofisi za TRA, Serikali iwatambue, iwasajiri kisha iwaajiri kama watoa huduma kwenye Kila ofisi wanakopatia riziki. Wamejitengenezea mfuko ambao ni wa hiali, kwa namna moja wanapunguza mahangaiko kwa wateja. Ukiiamua kuwakwepa uwe umejipanga kuchezeshwa nenda rudi.
Huko ni kulea uozo,Hawa watumushi wameajiriwa kwa ajili Gani, halafu siku utakapotibiwa na daktari kishoka ndo utakua umuhimu WA kuzingatia taalum
 
Huko ni kulea uozo,Hawa watumushi wameajiriwa kwa ajili Gani, halafu siku utakapotibiwa na daktari kishoka ndo utakua umuhimu WA kuzingatia taalum
Mkuu, kama Kuna Wana taaruma huko maofisini, kwa nini korido za TRA zimejaa vishoka? Kwa nini wana ushirikiano na hao unaowaita wataalamu? Ni Nani anayewalea vishoka huko maofisini kama ni watu hatari kiasi hicho?.
 
vishoka ni wazuri sana kwa jambo lako kumaliza mapema bila usumbufu
 
Back
Top Bottom