GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
"Leo nimegundua kuwa kumbe Mazoezi niliyoyafanya hayakuwa sahihi kwangu na nilipofika Kilomita ya 30; kuelekea ya 35 sikuona haja ya kuendelea hadi Kilomita 42 tulizokuwa tunakimbia, hivyo naomba radhi na asitafutwe mchawi, nitajitahidi katika mashindano yajayo," amesema Mwanariadha aliyejivunja (aliyeyakimbia) Mashindano ya Kimataifa ya Riadha Duniani Alphonse Felix Simbu.
Chanzo: Spoti Leo ya Radio One Usiku huu Saa 1 na Nusu hadi Saa 2 Kamili.
Kwanini GENTAMYCINE nimesema akamatwe na ahojiwe?
Kwanza kitendo cha kukata tamaa na kuachia njiani (tena akienda pembeni kabisa kujificha) ni kutudhalilisha Watanzania.
Pili, kauli yake kuwa amegundua hakufanya mazoezi sahihi yanakinzana na kauli yake aliyoitoa juzi na jana kuwa amejiandaa kikamilifu na atatuletea Medali Watanzania, matokeo anaenda kutuletea Medali ya Kuyatoroka Mashindano na kwenda Kujificha Porini kwa muda.
Tatu, binafsi kwa ninavyowajua viongozi wa michezo mbalimbali nchini Tanzania walivyo wajanja na matapeli (Panjuani na Samjo) huenda huyu Mwanariadha Alphonse Felix Simbu amepewa chake (pesa) kisha akaambiwa ajichomeshe (ajifelishe) kwa makusudi ili asiwe kikwazo kwa wanariadha wengi wakubwa waliokuwa wakimhofia kutokana na uimara wake.
Msichokijua
Wanariadha wote walioshiriki Mashindano haya huko Jijini Budapest nchini Hungary walipewa ratiba yote ya mashindano kuanzia eneo mpaka umbali na huyu mwanariadha aliomba msaada kutoka Serikalini ili kuweka kambi na kujiandaa kikamilifu huko huko Ulaya.
Ambapo alipewa na hata yeye mwenyewe kushukuru, ila leo kwa makusudi, uhuni na usanii anayaachia mashindano katikati tena kwa kutoroka na kuzamia (kuingia) porini (msituni).
Na alivyo mpuuzi (asivyo na akili) ameshindwa hata kudanganya kuwa alishikwa na tumbo la kuhara au haja kubwa (kuukweka) kwa ghafla kutokana na kufakamia hovyo vyakula vya Wazungu muda mchache kabla ya kuanza mashindano. Yeye kaona atudanganye kuwa hakuwa na mazoezi ya kutosha!
Asitufanye Watanzania wote wajinga.