Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 13,741
- 13,049
Kwa mujibu wa Askofu Pengo huyu Gavana wa Dar es salaam ndiye Rais ajaye.Siyo kwamba najigamba au kujidai. Ni ukweli tu. Ukweli kwamba, katika watu waliom-‘define’ huyu ‘Gavana’ wa Dar es Salaam humu jukwaani, basi mimi ni mmoja wa watu walio juu katika orodha ya watu hao.
Hizi siku mbili tatu nimejiuliza maswali mengi sana.
Mojawapo ni hili: hivi huyu Rais wetu anakwama wapi?
Manake haiingii akilini kabisa. Kuna watu wengi tu ambao kawatumbua ‘unceremoniously’ kwa makosa madogo kabisa yasiyo stahili hata kuwa sababu ya mtu kutumbuliwa.
Lakini ikija kwa huyu ‘Gavana’, licha ya makosa yake yote, Rais mpaka leo hajamtumbua.
Mpaka Wamarekani nao wameona. Si ajabu wameona siku nyingi tu lakini wakawa wanavuta muda kuona kama Rais atatumia madaraka yake na kutenda [kumtumbua], lakini wapi.
Wamesubiri mwishowe na wao wamechoka. Sasa wameamua kutenda kwa kadri wawezavyo.
Huyu Rais wetu huyu...kama somo halielewi, ina maana na picha nayo haioni?
Anakwama wapi huyu Rais wetu?
Haya, pale wizara ya mambo ya nje kamtoa waziri ambaye ni mwanadiplomasia mbobezi halafu kamweka Kabudi!
Huyu Kabudi ataweza kweli ku ‘navigate the murky waters of diplomacy’?
Ona alivyoenda Kenya kwenye ule uzinduzi wa ripoti yao ya BBI!!
Kaenda katoa mahubiri utadhani huko alikotoka ni peponi.
Kilichotokea kwa ‘gavana’ sidhani kama kimewahi kutokea [unprecedented].
Ila sasa kimetokea. Chini ya utawala wa Magufuli.
Magufuli anakwama wapi? Hana hekima? Busara?